Wakati Watanzania wakiadhimisha Siku ya Kumbukizi ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Waziri Mkuu mstaafu Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda ameadhimisha siku hii jijini Beijing China kwa kuhutubia katika Chuo Kikuu cha Peking pamoja na viongozi wa Serikali, Chama cha Kikomunisti, Wanadiplomasia, Wanazuani na wanafunzi.
Mwalimu Nyerere alijenga urafiki mkubwa wa Tanzania na China wakati wa uongozi wake. Miongoni mwa ushirikiano mkubwa uliofanywa na nchi hizi mbili uliwezesha China kufanya ujenzi wa Reli ya TAZARA iliyounganisha Tanzania na Zambai iliyokuwa chini ya uongozi wa Rais Keneth Kaunda.
Aidha, China ilijenga kwa pamoja na Tanzania walijenga Kiwanda kikubwa cha nguo kilichopewa jina la URAFIKI (Urafiki Textile). Urafiki wa Tanzania na China umeendelea kudumu katika katika awamu zote za uongozi wa Tanzania kwenye maeneo mbalimbali ya biashara, uwekezaji, elimu, uchumi na kadharika.
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye ni muasisi wa Taifa la Tanzania alizaliwa mwaka 1922 na kufarikai dunia tarehe 14 Oktoba, 1999 akiwa nchini Uingereza alipokwenda kwa ajili ya matibabu. Leo imepita miaka 20 tangu Mwalimu Nyerere alipofariki dunia.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.