Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa katika kutekeleza jukumu lake la Msingi la rasilimali fedha na mapato katika mamlaka ya Serikali za Mitaa kupitia kwa wataalam wa TEHAMA iliandika andiko kuomba uboreshaji wa mifumo ya Unadaaji wa Mipango na Bajeti (PlanRep) na ule wa utoaji wa taarifa za fedha kwenye vituo vya kutolea huduma (FFARS) lilikubaliwa na mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) unaoendeshwa chini ya ufadhili wa USAID na kutokana na umuhimu wa mifumo hii, PS3 sasa itatekeleza mradi huu katika Halmashauri zote 185 nchini tofauti na zile 93 ambazo zimeainishwa kwenye mripango yao huku uzinduzi ukitarajiwa kufanywa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa Septemba 05, 2017 katika ukumbi wa mikutano wa LAPF Mjini Dodoma.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo kwa maafisa TEHAMA Mjini Dodoma leo, Mkurugenzi msaidizi wa Miundombinu ya TEHAMA wa Ofisi ya Rais TAMISEMI Baltazali Kibola amesema Mifumo hiyo kwa sasa imekamilika na imekwishajaribiwa na kuhakikiwa tayari kwa kuanza kutumika katika Halmashauri zote nchini.
Ukamilishwaji wa mifumo hii unaondoa kabisa mifumo ile ya awali iliyokuwa ikitumika katika mamlaka za Serikali za Mitaa na yametolewa mafunzo kwa wataalam wa TEHAMA, Madaktari Wakuu wa Halmashauri, makatibu wa afya, Maafisa Mipango na Wahasibu kuanzia ngazi ya Mkoa, Halmashauri na kutoka katika ngazi za vituo vya kutolea huduma ili kuhakikisha kwamba hawakutani na changamoto zozote katika matumizi ya mifumo hii iliyoboreshwa.
Naye Mkuu wa Timu ya Rasilimali Fedha kutoka PS3 Dr. Gemini Mtei amesema mradi huu utatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano na una lengo la kuboresha mifumo ili iweze kuendana na hali ya sasa na mahitaji yaliyopo na kwa hakika mradi huu utamaliza kabisa matumizi mabaya ya fedha za Umma na thamani ya Fedha itaonekana katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Mamlaka ya Serikali za Mitaa Nchini kwa kipindi kirefu zimekuwa zikikabiliwa na changamoto ya mifumo kadha wa kadha ikiwa ni pamoja na ile ya uandaaji wa Bajeti na Mipango sambamba na ule wa uandaaji wa taarifa za fedha katika vituo vya kutolea huduma.
Changamoto ilipelekea matumizi makubwa ya fedha za umma na upotevu wa muda mwingi kwa watumishi wanaohusika na maandalizi ya bajeti kwa kuwa hutumia muda mrefu katika maandalizi hayo na kupelekea wananchi wengi kukosa huduma kutokana na kutokuwepo katika vituo vya kazi kipindi chote cha maandalizi ya bajeti.
Mfumo uliokuwa ukitumika hapo awali ujulikanao kama ‘Planning and Reporting‘ ukimaanisha Uandaaji wa Mipango na Utoaji wa Taarifa, mfumo huu haukufanya vizuri katika eneo la utoaji wa taarifa, hivyo ilikuwa vigumu kupata taarifa sahihi na kwa wakati za utekelezaji wa bajeti katika halmashauri husika.
Sambamba na hilo changamoto kubwa ilikuwa katika vituo vya kutolea huduma kwani matumizi ya Fedha zinazopelekwa katika vituo hivyo hayaendani na miradi inayotekelezwa na pia wananchi wamekosa huduma bora kutokana na mfumo uliokuwepo kutowabana wahusika kuzingatia matumizi bora ya Fedha za Serikali.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.