Serikali imezitaka Halmashauri zote nchini kutambua kuwa jukumu la kusafisha barabara na mitaro ni la kwao na si la Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) huku wananchi wakihimizwa kuzitunza barabara zinazojengwa katika maeneo yao.
Rai hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- TAMISEMI anayeshughulikia miundombinu Mhandisi Rogatus Mativila wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa barabara na madaraja zilizojengwa kwenye kata ya Kibakwe wilayani Mpwapwa.
Mhandisi Matavila alisema kwamba Halmashauri zielewe kwamba suala la kusafisha barabara zilizojengwa kwenye Halmashauri, Miji na Majiji yao ni jambo la kwao na hivyo wanatakiwa kuhamasishana waweze kusafisha.
“Tumeshaletewa barabara nzuri tuzitunze ili zitusaidie sisi wenyewe, mwananchi una nyumba hapo pembeni ya barabara ni vyema kujitoa kusafisha hizo nyasi kandokando ya barabara”, alisisitiza
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.