HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imekamilisha ujenzi wa madarasa ya sekondari katika shule 23, ambapo imejenga jumla ya vyumba 29 na ofisi Jiji la Dodoma ilipokea kiasi cha shilingi milioni 580 kutoka serikali kuu, ili ifikapo Januari 2023 watoto wote waingie madarasa yakiwa yamekamilika.
Ameyasema hayo Mkurugenzi wa jiji la Dodoma Joseph Mafuru wakati akikabidhi madarasa hayo 29 na ofisi 24 kwa mkuu wilaya ya Dodoma leo katika shule ya sekondari
‘‘Kazi yetu imekamilika kuanzia tarehe moja mpaka mbili ya mwezi desemba’’. Alisema Mkurugenzi
Aidha, pamoja na madarasa 29 pia kuna ofisi za mwalimu 24, Ambapo kwenye ramani, tamisemi ilitoa nafasi ya darasa pamoja na ofisi yake,.
"Ni ujenzi mmoja ambao ni mzuri aliendelea kusema kuwa, uwepo wa ofisi katikati mwa madarasa mawili inafaida, Moja tunakuwa na ofisi za kutosha na kupunguza msongamano wa walimu katika ofisi, mbili ile kazi ya kukaa kwenye ‘pool’ walimu inaleta shida sana ya tatu ni uthibiti wa nidhamu ya wanafunzi". Alisema Mafuru
Aliendelea kusema kuwa mazingira ambayo Jiji imepanga ni kuwa Mtoto atakaeingia katika darasa ambalo tumejenga anatofauti na mtoto anayesoma ‘martin luther’ au ‘Ignatus’,kwa kuwa madarasa yametengenezwa kwa ubora.
Halmashauri ya jiji la Dodoma inamshukuru Rais Dtk. Samia Suluhu Hassan katika kuimarisha elimu ya sekondari kwa kujenga madarasa 29 na ofisi ndogo za walimu 24.
‘‘Watoto watakapo fungua shule Januari wanakwenda kusoma katika mazingira safi na salama’’.
Alimalizia kwa kutoa wito kwa wazazi na viongozi wa mitaa na kata kuhakikisha watoto wanahudhuria shule.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.