Na. Faraja Mbise, NZUGUNI
Halmashauri ya Jiji la Dodoma inaendelea kutoa shukrani kwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutenga fedha kwa ajili ya maboresho ya miundombinu ya sekta ya afya kwa kipindi chote cha miaka minne ya uongozi wa awamu ya sita inayopelekea huduma bora kwa wananchi.
Hayo yalizemwa na Mganga Mkuu wa Jiji la Dodoma, Dkt. Sebastian Pima wakati akiwasilisha taarifa fupi ya Zahanati ya Mahomanyika kwa Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Dodoma iliyofanya ziara ya kutembelea zahanati hiyo.
Dkt. Pima alisema “tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutenga fedha kwa ajili maboresho ya miundombinu ya sekta ya afya”.
Akizungumza kuhusu historia ya zahanati hiyo, alisema kuwa mwaka ambao zahanati hiyo imejengwa na jumla ya watumishi waliopo wanaowahudumia wananchi wa Mtaa wa Mahomanyika. “Zahanati ya Mahomanyika ilianzishwa mwaka 1992 na inapatikana katika Kata ya Nzuguni. Zahanati hii ina jumla ya majengo mawili yambayo ni jengo la wagonjwa wa nje (OPD) na nyumba ya watumishi. Pia ina jumla ya watumishi watatu ambao ni mganga mmoja na wauguzi wawili, tuna mahitaji na watumishi 15. Kwahiyo, upungufu ni watumishi 12, alisema Dkt. Pima.
Halmashauri ya Jiji la Dodoma, imetenga fedha kwenye bajeti ya mwaka 2025/2026 kwa ajili ya kuanzisha ujenzi wa jengo jipya lenye muunganiko na jengo la wazazi kwa lengo la kusogeza huduma bora za afya karibu na wananchi.
Habari hii imehaririwa na Dennis Gondwe
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.