HALMASHAURI zote nchi zimetakiwa kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za kuhifadhi na kusimamia mazingira katika maeneo yao.
Agizo hilo limetolewa leo na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mwita Waitara kwa nyakati tofauti alipofanya ziara mkoani Tabora.
Akiwa katika ziara hiyo Waitara alisema kuwa kwa kutenga fedha hizo kutazisaidia halmashauri hizo kuweza kupata vitendea kazi vitakavyotumika katika usafi wa mazingira.
“Huwezi kusema unazoa taka wakati huna hata vitenfdea kazi kwa hiyo halmashauri zinapaswa kutenga asilimia kumi ya bajeti zao kwa mwaka na kuweka mikakati ya kutunza mazingira,” alisema.
Aidha alitoa wito kwa halmashauri zote kuhakikisha vinaundwa vikundi vitakavyojishusisha na uzoaji taka mitaani ili kuweka maeneo yao katika hali ya usafi.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.