HALMASHAURI nchini zimehimizwa kuchangamkia fursa za uwekezaji ikiwamo madini, uvuvi, utalii, ufugaji na kilimo kwa kuanzisha kampuni na miradi ya kimkakati itakayosaidia kujikwamua na ukata wa fedha badala ya kutegemea mapato yatokanayo na tozo za ushuru na fedha kutoka Serikali kuu.
Hayo yamesemwa na Afisa Biashara na Mratibu wa dawati la uwekezaji mkoani Mara, Gambales Timotheo wakati akiwasilisha mada ya fursa za uwekezaji zilizopo mkoani Mara kwenye mafunzo ya kuwejengea uwezo Wakurugenzi na Wenyeviti wa Halmashauri juu ya uundaji wa kampuni na utambuzi wa miradi itakayosaidia kukuza uchumi wa Halmashauri hizo.
Mafunzo hayo maalum yameandaliwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa (UNDP) kwa kushirikiana na Serikali na Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini (IRDP).
Chanzo:ITV Tanzania (facebook)
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.