MKURUGENZI wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi ametoa wito kwa Halmshauri nchini kuwekeza katika Manispaa ya Dodoma kama njia mojawapo ya kujiongezea mapato ya ndani.
Ametoa wito huo jana wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara ya mafunzo ya Madiwani na Wataalam wa Manispaa ya Kigamboni Mkoa wa Dar es Salaam waliyoifanya katika Manispaa ya Dodoma.
Kunambi aliwaeleza wageni hao kuwa, Manispaa ya Dodoma ina fursa nyingi za uwekezaji ikiwa ni pamoja na ujenzi wa hoteli za kisasa, majengo ya Ofisi, na miundombinu mingine ikizingatiwa kuwa kuna rasilimali ardhi ya kutosha na sasa ni Makao Makuu ya Nchi.
Msafara wa watu 20 wakiwemo Madiwani na Wataalam kutoka Manispaa ya Kigamboni ukiongozwa na Meya wa Manispaa hiyo Mstahiki Maabad Hoja walifanya ziara ya mafunzo juu ya usafi wa Mazingira na uhifadhi wa taka kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya kuzika taka ardhini (Land Filling) ambapo Manispaa ya Dodoma inafanya vizuri kupitia Dampo lililopo katika Kata ya Ntyuka katika Manispaa hiyo.
Pia ziara yao ililenga kulijifunza kuhusu suala la utozaji na ukusanyaji wa kodi mbalimbali unaofanywa na Manispaa.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.