Na. Hellen M. Minja,
Habari – DodomaRS
Halmashauri chini ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI, leo Februari 07, 2025, zimetekeleza agizo la Rais wa Tanzania kwa kusaini Mikataba na benki washirika inayohusu utoaji wa mikopo inayotokana na 10% ya mapato ya ndani ya Halmashauri hizo ambayo hutolewa kwa vikundi vya Wanawake,Vijana na Watu wenye ulemavu.
Hafla hiyo ya utiaji saini, imefanyika baina ya benki tatu washirika ambazo ni NMB, CRDB na Uchumi Commercial Bank na Halmashauri 10 zilizowakilisha Halmashauri nyingine 175 za Mikoa yote ya Tanzania Bara katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma jengo la Mkapa Jijini humu.
Waziri mwenye dhamana Mhe. Mohamed Mchengerwa, amesema huo ni utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais la kuangalia namna bora ya utoaji wa mikopo hiyo ili fedha hizo ambazo zimelengwa kuyakomboa makundi maalumu ziweze kuleta tija.
“Katika kutekeleza maelekezo hayo, ilionekana kuwa mikopo hii itolewe katika mifumo ya kibenki na mifumo iliyoboreshwa na ilionekana Serikali ianze kutoa mikopo hiyo kwa kushirikiana na Mabenki lengo likiwa ni kuongeza ufanisi katika usimamizi na kuibua yale yanayowasibu Watanzania wa kawaida, wanyonge na wenye vipato vidogo.”
Aidha, ameongeza kuwa, zaidi ya shilingi 234,000,000,000 ambazo ndio kiwango cha juu kabisa, zinatarajiwa kutolewa kwa njia ya mikopo na zinakusudiwa kwenda kwa wananchi wa chini kabisa kwa lengo la kuinua uchumi wao, vikundi na Taifa kwa ujumla.
Nae, Katibu Mkuu TAMISEMI Bw. Adolf Ndunguru, amesema “matamanio ya Mhe. Rais ni kuona ufanisi umeboreshwa katika utoaji wa mikopo hii ambayo aliitolea maelekezo yake mwezi Machi, 2023, hivyo ni mwanzo wa mapinduzi makubwa katika kuhakikisha inaleta matokeo yenye tija kuliko huko nyuma”.
Akitoa salamu za Mkoa wake, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amewakaribisha wageni Mkoani hapa na kuwasihi kuchangia uchumi wa Mkoa kwa kununua bidhaa za Dodoma pamoja na kutembelea miradi mikubwa ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa hapa Makao Makuu ya nchi.
Vilevile, benki washirika wameishukuru Serikali kwa kuwachagua kwenye mradi huo na watahakikisha wanufaika wanapata mikopo kwa wakati na wale wenye vigezo wanahudumiwa kwa wakati pia huku
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.