WAZIRI wa Afya Mhe Ummy Mwalimu ameagiza Halmashauri zote nchini kuajiri Wataalamu wa Afya wa Mikataba ili kuongeza nguvu ya kutoa huduma bora na haraka kwa Watanzania.
Waziri Ummy alitoa agizo hilo alipokuwa anaongea na Timu ya usimamizi wa Afya ya Mkoa pamoja na Wataalamu wa Afya ngazi ya Jamii kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wakati wa ziara yake Mkoani humo.
“Naagiza Halmashauri zote nchini kuajiri Wataalam wa Afya wa Mikataba ili tuendelee kutoa huduma bora Kwa Watanzania na kwa haraka". Alisema Mwalimu
Aidha, Waziri Ummy alitaka huduma bora za uangalizi kwa watoto wachanga (NICU) ziwepo katika Hospitali za Halmashauri zote nchini ili tuokoe maisha ya Watoto.
“Maelekezo yangu nataka kila kila Hospitali ya Halmashauri zitoe huduma za uangalizi kwa watoto wachanga (NICU) sababu tunataka kila mzazi anaekwenda kujifungua katika Hospitali atoke na mtoto wake”. Aliongeza Mwalimu .
Pia, Mwalimu alisema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshafanya jukumu lake la kutoa fedha katika Sekta ya Afya na Sasa ni jukumu la Wataalam wa Afya kutoa huduma bora kwa watanzania.
“Tunamshukuru sana Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kujali Afya za Watanzania ametoa fedha za majengo, ametoa fedha za vifaa na vifaa tiba, fedha za dawa sasa ni jukumu letu sisi watendaji kutoa huduma bora kwa Watanzania”. Alisema Mwalimu
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.