Na. Getruda Shomi, DODOMA.
MWAKILISHI wa mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Fatuma Mganga amezitaka Taasisi za kusimamia haki za binadamu na zile za msaada wa kisheria kuweka utaratibu wa kuwafikia wananchi wa vijijini ili waweze kunufaika na huduma zao.
Aliyasema hayo alipokuwa akikagua mabanda ya maonesho katika maadhimisho ya miaka 20 ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora yanayofanyika katika viwanja vya Jakaya Kikwete Convetion Center.
Mganga alisema kuwa Taasisi za msaada wa kisheria zisiishie tu mijini bali kuwepo na njia nzuri ya kuwafikia wananchi walioko vijijini ili nao waweze kupata msaada wa kisheria.
“Wekeni nia madhubuti ya kuwafikia wananchi wa vijijini ili nao wajue mnatoa huduma zenu bure, nao wapate msaada wa kisheria” alisema Mganga.
Aidha, Mganga aliongeza kuwa Taasisi za kisheria zinapowafadhili mawakili katika utoaji wa msaada wa kisheria lazima kuwe na ufatiliaji ili kusudi la kuwatetea walengwa liweze kufanikiwa na wapatiwe haki zao.
“Wekeni njia Madhubuti yakuhakikisha mnawafikia wananchi wote na kuwafatilia wale mnaowawezesha kama kweli wanafanya kazi hizo za kuwafikia na kutoa msaada wa kisheria kama taasisi zenu zinavyolenga kufikisha huduma hizi kwa jamii”
Hata hivyo Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Amina Talib aliongeza kuwa kuna Taasisi hazifanyi vizuri zina udanganyifu katika utoaji wa huduma hivyo muwe na ufatiliaji.
“kuna Taasisi zinaudanganyifu muwe na ufatiliaji na kujua kama wanawafikia wananchi kweli”alisema Talib.
Naye Mtapa Wilson, Afisa mawasiliano wa Taasisi ya “Legal Service Facility” alielezea kuwa Taasisi yao hufanya mapitio, tathimini na ufatiliaji wa moja kwa moja kwa wale wanaowawezesha katika kutoa msaada wa kisheria kwa jamii.
“tunautaratibu wakufanya mapitio, tathimini na ufatiliaji kwa wale tunaowawezesha ili kuona kama kweli msaada wetu unatumika vizuri na kuwafikia wananchi kweli”
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.