MWENYEKITI wa Bodi ya Hazina Saccos, Bw. Aliko Mwaiteleke, amesifu utekelezaji wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma jinsi inavyoshughulikia mchakato wa uuzaji viwanja katika Jiji la Dodoma.
Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti huyo wakati akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali yaliyojiotokeza kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa chama hicho baada ya kutoa taarifa ya utekelezaji ya shughuli za Chama cha Ushirika wa Akiba na Mikopo cha Hazina (Hazina SACCOS), unaofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Karimjee Jijini Dar es Salaam.
Jiji la Dodoma linafanya vizuri katika mchakato wa uuzaji wa viwanja na utoaji wa hati, maana tumeshughulikia viwanja vya wanachama wetu katika maeneo ya Nzuguni, Nala na Iyumbu na mambo yameenda vizuri.
"Napenda kuwajulisha kuwa tupo hatua za mwisho kwenye mradi wa Nzuguni ambao ramani imekwishakamilika. Wanachama wengi wameshachukua hati zao za miradi ya awali na wachache bado hawajachukua, lakini Hati zipo ofisini”. Amesema Bw. Mwaiteleke.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.