Asila Twaha, OR- TAMISEMI
Mabingwa wa tetezi kombe la Ligi ya Muungano mchezo wa netiboli Tamisemi QUUENS wameendelea kutwaa ubingwa kwa mwaka 2023 kwa kumaliza mechi na kuwafunga wahasimu wake timu ya Arusha Polisi goli 64-33.
Mechi iliyochezwa katika viwanja vya Gymkhana katika visiwa za Zanzibar TAMISEMI QUUENS wameendelea kupambania kombe lao na kuhahakisha linarudi tena kwa mwaka 2023.
TAMISEMI QUEENS ilipangiwa kucheza mechi kumi na timu walizokutana nazo ni pamoja na timu ya Mafunzo ZNZ, JKU, ZNZ, NSSF DSM, JESH STAR,Uhamiaji DSM,JKT DSM, Zimamoto ZNZ,ZNZ worries, KVZ na Polisi Arusha na timu zote hizi waliibuka na ushindi na mpaka wanachukua ubingwa wameshinda pointi 20.
Kwa upande wa kocha wa Timu ya TAMISEMI QUEENS Maimuna Kitete ameushukuru uongozi wa Tamisemi kwa kuendelea kuisimamia timu hiyo kimaadili na kuiwezesha kuhakikisha timu hiyo inakuwa vizuri katika michezo yao.
Amefafanua siri ya kuendelea kufanya vizuri katika mechi zao ni sababu ya kuwa na umoja,ushirikiano na nidhamu ya wachezaji hao lakini pia ni ushirikiano mkubwa wanaoupata kutoka kwa viongozi wa TAMISEMI.
Timu ya TAMISEMI QUEENS imeendelea kuwa mabingwa wa ligi ya Muungano kuanzia mwaka 2021 hadi sasa.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.