Hifadhi ya Taifa ya Serengeti imeshinda tuzo ya kuwa hifadhi bora katika Bara la Africa kwa mwaka 2020. Tuzo hizo zimetangazwa jana Novemba 9, 2020 na Taasisi ya World Travel Awards (WTA) ya nchini Marekani kwa njia ya mtandao.
Hii ni mara ya pili kwa Hifadhi ya Taifa Serengeti kushinda katika kundi la Hifadhi zinazoongoza kwa ubora zaidi Barani Afrika baada ya kushinda pia mwaka 2019.
Serengeti imeibuka na ushindi katika shindano hilo lililoshindanisha hifadhi nyingine za Central Kalahari (Botswana), Etosha (Namibia), Kidepo Valley (Uganda), Kruger (Africa ya Kusini) na Maasai Mara National Reserve (Kenya).
Serengeti inajivunia umaarufu wa msafara wa nyumbu wanaohama zaidi ya milioni moja na nusu, aina mbalimbali za wanyamapori wanaopatikana kwa wingi, madhari nzuri ya kuvutia pamoja na shughuli mbalimbali za utalii zinazovutia watalii wengi.
Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) linaishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wananhi,Wadau wa utalii pamoja na wale wote waliotumia muda wao kupiga kura na kuifanya Serengeti kuwa mshindi wa Hifadhi bora zaidi kwa Bara la Afrika kwa mwaka 2020.
Chanzo: Pascal Shelutete - Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi - Mawasiliano
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.