Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu ameupa uongozi wa Mkoa wa Mara wiki mbili kuhakikisha huduma za afya zinaanza kutolewa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara (Kwangwa) baada ya ujenzi wake kufikia zaidi ya asilimia 90.
Hospitali hiyo iliyoanza kujengwa mwaka 1977 na hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere imekuwa ikisuasua kwa muda mrefu mpaka Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ilipotoa Tshs. Bilioni 15.8 ambazo zimetolewa kwa awamu ili ziweze kukamilisha Hospitali hiyo na kuanza kutoa huduma kwa wananchi wa Mara na miko ya jirani.
Huduma zitakazopatikana hapo ni pamoja na huduma za kibingwa za mifupa na ubongo, kusafisha figo (Dialysis) na nyinginezo.
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu alipotembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara (Kwangwa) kuona maendelea ya ujenzi wa Hospitali ambao umefikia asilimia 90.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.