Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa ametembelea Hospitali mpya ya Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha ambayo itatumika kulaza watakaobainika kuwa na virusi ya ugonjwa wa Corona (Covid-19). Mhe. Kassim Majaliwa amesema hospitali hiyo itatumika kulaza watu walioambukizwa ugonjwa huo na kwamba itatumika kwa muda na baada ya ugonjwa huo kwisha itaanza kutoa huduma nyingine nza afya.
Waziri Mkuu aliwaeleza wananchi wa Wilaya a Kibaha kuwa watu wenye maambukizi ya virusi vya COVID-19 watalazwa katika hospitali hiyo kwa muda wa siku 14 na baada ya uchunguzi ikibainika hawana ugonjwa huo wataruhusiwa kurejea nyumbani.
Mhe. Kassim Majaliwa amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya Corona na amezikumbusha familia kuwa na utaratibu wa kunawa mikono mara kwa mara kwa kutumia maji tiririka na sabuni au kutumia vitakasa mikono (sanitizer). Awali, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu alimweleza Waziri Mkuu kwamba hospitali hiyo ilipokea kiasi cha nshiling milini 394 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa hospitali hiyo.
Baadhi ya majengo ya Hospitali ya Wilaya ya Kibaha ambayo itatumika kwa matibabu ya watu wakataobainika kuambukizwa ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayoenezwa na virus vya Corona ujulikanao kama Covid-19.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.