• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Waziri Ummy azitaka Hospitali za Rufaa za Mikoa kuwa na vifaa muhimu vya kutolea huduma

Imewekwa tarehe: July 2nd, 2019

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amewataka Waganga Wafawidhi wa Hospitali za Rufaa za Mikoa nchini kuhakikisha wanakua na vifaa vya muhimu vya kutolea huduma za afya kwa wagonjwa wanaofika Hospitalini kupata matibabu.

Waziri Ummy amesema hayo wakati akifungua mkutano wa viongozi wa Hospitali za Rufaa za Mikoa unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha Mipango Jijini Dodoma.

Waziri Ummy amewataka Waganga Wafawidhi hao kubainisha aina ya vifaa vya matibabu vinavyotakiwa kupelekwa katika Hospitali  zao ili kuhakikisha mgonjwa anapofika Hospitalini hakosi huduma wakati anapoenda kupata matibabu.

“Mganga Mfawidhi unatakiwa useme vifaa gani ukivipata utaboresha huduma, hatutaki mgonjwa afike Hospitali halafu akose huduma, boresha kwanza kupata vifaa vya msingi kabla ya vile vikubwa kama CT-Scan”. Amesema Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy amesema lengo la Wizara ya Afya chini ya Serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha huduma bora za afya zinatolewa ili mwananchi akifika katika Hospitali za Rufaa aseme kweli huduma zimeboreshwa.

“Lengo la Serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha kila Hospitali ya Rufaa inakua na huduma za kipaumbele 13 zikiwepo huduma za mama na mtoto ili kusaidia kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na magonjwa mengine ambayo yanaweza kutibiwa bila kumpa rufaa mgonjwa”. Ameongeza Waziri Ummy.

Kwa upande wake, Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amewataka Waganga Wafawidhi wa Hospitali za Rufaa za mikoa kuhakikisha wanasimamia vizuri ukusanyaji wa mapato kwa kufunga mfumo utakaotumika kukusanya mapato na kuachana na makaratasi.

“Tuendelee kuboresha huduma za afya na kusimamia ubora wa huduma tunazozitoa na kuboresha upatikanaji wa vifaa na kuwa wabunifu japokuwa tuna changamoto za rasilimali watu ila huduma za kibingwa ziboreshwe ili kupunguza rufaa za nje”. Amesema Dkt. Ndugulile.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Zainab Chaula amewataka Waganga Wafawidhi hao kuhakikisha wanaripoti taarifa za maendeleo ya Hospitali na atakayeshindwa kufanya hivyo hataendelea na uongozi. Pia amewataka Waganga Wafawidhi hao kuwa na ushirikiano ili kufanya sekta ya afya kuwa ya mfano.

“Tuhakikishe tunaweka mifumo vizuri ya kutoa huduma kwa wahitaji kuanzia ngazi ya chini kwa kufuata miongozo na mikataba iliyotolewa, na tufanye kazi kwa ushirikiano bila kujali cheo au nafasi ya mtu”. Amesema Dkt. Chaula.

Pamoja na hayo katika Mkutano huo Waziri Ummy alizindua muongozo wa uendeshaji wa Hospitali za Rufaa za Mikoa pamoja na jarida la afya ya jamii toleo la kwanza.

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu alifurahia muongozo wa uendeshaji wa Hospitali za Rufaa aliouzindua mapema leo, kulia ni Mkurugenzi wa Tiba Dkt. Grace Maghembe, akipokea muongozo huo kutoka kwa katibu Mkuu Dkt. Zainab Chaula na katikati ni Naibu waziri Dkt. Faustine Ndugulile akishuhudia.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akionesha jarida la afya ya jamii toleo la kwanza alilozindua wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Waganga Wafawidhi wa Hospitali za Rufaa za Mikoa unaoendelea jijini Dodoma. Kushoto ni Naibu Waziri Dkt. Faustine Ndugulile na Kulia ni Katibu wa Afya Dkt. Zainab Chaula.

Viongozi mbalimbali wa Wizara ya Afya na TAMISEMI wakiongozwa na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu wakionesha jarida la afya ya jamii toleo la kwanza lililozinduliwa leo na Waziri Ummy.


Chanzo: Blog ya Wizara ya Afya (www.afyablog.moh.go.tz)

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.