"...hapa Dodoma tumepanga kujenga barabara ya mzunguko ya njia nne yenye urefu wa kilometa 110 ambapo makandarasi wawili tayari wameshapatikana na ujenzi utaanza hivi karibuni"
Hayo yamesemwa na Rais Dkt. John Magufuli jana ikiwa na sehemu ya hotuba yake yenye kuonesha mwelekeo wa utekelezaji wa Serikali ya awamu ya tano katika kipindi chake cha pili.
" Tutakamilisha ujenzi wa kilometa 2,500 za lami na kuanza ujenzi wa barabara za lami zenye urefu wa kilometa 6,006 najua Wabunge wengi mmetoa ahadi za barabara za lami kwenye maeneo yenu,
Ili hatimaye tuweze kufikia lengo letu la kuunganisha Mikoa na Wilaya kwa barabara za lami, barabara hizo zimetajwa kwenye ilani yetu ya Uchaguzi na nyingine zinatokana na ahadi tulizozitoa katika kipindi cha Kampeni." alisema Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
Tumepanga pia kukamilisha ujenzi wa madaraja saba na kuanza madaraja mengine 14, ikiwemo daraja la Busisi, Wami na Pangani " Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
Zaidi ya hapo tutaendelea kushughulikia tatizo la msongamano wa magari kwenye Miji na Majiji yetu hususan Arusha, Dar es Salaam, Mbeya, Mwanza na hapa Dodoma ambapo tumepanga kujenga barabara ya mzunguko ya njia nne yenye urefu wa kilometa 110 ambapo Makandarasi wawili tayari wamekwishapatikana na ujenzi utaanza hivi karibuni" alifafanua zaidi Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika hotuba yake hiyo iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu kubwa na wabunge pamoja na wananchi.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.