• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Huduma za Afya Tembezi liwe jukumu la pamoja - Dkt. Gwajima

Imewekwa tarehe: June 25th, 2019

Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya, katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Dorothy Gwajima amewataka wadau wote wanaotoa Huduma Tembezi za Afya kuunganisha nguvu kwa pamoja ili huduma hiyo iweze kufikishwa katika Halmashauri zote nchini.

Dkt. Gwajima ameyasema hayo wakati wa kikao cha wadau wa Afya kuwasilisha taarifa mbalimbali za utekelezaji wa miradi kilichofanyika katika Ukumbi wa Takwimu Jijini Dodoma.

Akizungumza katika kikao hicho Dkt. Gwajima amesema Huduma Tembezi za Afya ni muhimu kufikishwa katika ngazi ya jamii ili wananchi waweze kupata matibabu kutoka kwa madaktari bingwa tena kwa gharama nafuu.

“Huduma hizi zimekuwa zikitolewa na taasisi tofauti kwa nyakati tofauti na kila taasisi inalenga eneo fulani ambalo inachagua hivyo kuna maeneo ambayo yamekuwa yakinufaika na huduma hizi mara kwa mara lakini kuna sehemu nyingine hazifikiwi kabisa, sasa umefika wakati wa kukaa pamoja na kuunganisha nguvu ya wadau wote pamoja na Serikali na kupelekwa huduma hii katika Halmashauri zote ili kila mwananchi mwenye uhitaji anufaike nayo”

Kupitia kikao hiki cha leo tutaunda kamati ya uendeshaji ambayo itahusisha wataalamu wa OR-TAMISEMI, Wizara ya Afya, asasi zisizo za kiserikali pamoja na wadau wanaotekeleza afua za Afya ambao watakuja na hadidu za rejea zitakazotuongoza katika kutekeleza azima yetu hii kwa ufanisi, aliongeza Dkt. Gwajima.

Aidha, Dkt. Gwajima alisema kuwa “tunajua tuna vituo vya kutolea huduma lakini si wakati wote vituo hivyo vinakuwa na madaktari bingwa, na kwa mwananchi wa kawaida kusafiri mpaka kukutana na madaktari bingwa ni gharama hivyo tukisogeza huduma hizi tutawatibu wananchi wetu hata yale magonjwa ambayo walikuwa wameyakatia tamaa” alisema Dkt. Gwajima.

Dkt. Gwajima aliongeza kuwa Huduma hizi tembezi zina faida zake, kwanza gharama za kuwekeza katika huduma hii ni ndogo lakini inawafikia watu wengi tena kwa muda mfupi. Unafuu huu wa gharama sio kwa sisi kama watoa huduma lakini pia kwa wagonjwa ambao ndio wanufaika wa huduma hii yaani ugonjwa ambao angeweza kutumia zaidi ya shilingi milioni moja anaweza kupata huduma hiyo hiyo kupitia kliniki tembezi kwa elfu thelathini tu.

“Huduma Tembezi ni msaada kwa wanyonge, wananchi wanaugua magonjwa makubwa ambayo hata akisafiri kumfuata daktari bingwa anaweza akafia njiani kabla hata hajakutana na huyo daktari, kupitia huduma hii watakutanishwa na madaktari bingwa kwa urahisi na nafuu zaidi na hapo tutakuwa tumegusa maisha ya watanzania na kuwaongezea siku za kuishi maana wangeweza kufa kwa kukosa huduma za Afya stahiki kwa magonjwa yanayowasumbua” alisema Dkt. Gwajima.

Tusipowafuata na kuwatibu wananchi wataendelea kunywa miti shamba na kwenda kwa waganga wa kienyeji na hata wakati mwingine kupoteza maisha yao kwa kukosa matibabu stahiki. Hebu tuwafikie wote kupitia huduma hii ya kliniki tembezi, alimalizia Dkt. Gwajima.

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainabu Chaula amesema agenda kuu katika sekta la Afya ni huduma ya Afya kwa wote na hakuna mtu atakayeachwa nyuma hivyo ni lazima tuifikishe huduma hii ya kliniki tembezi kwa wananchi wote.

“Tunapoelekea katika uchumi wa kati ni wajibu wetu kuhakikisha kila mwananchi anakuwa na Afya njema ili aweze kushiriki kikamilifu katika kujitafutia kipato, sasa hii kazi kwetu. Itakua rahisi tukiunganisha nguvu na rasilimali katika kutoa huduma hii ya Afya tembezi, tushirikiane kikamilifu kuleta tabasamu kwa watanzania” alisema Dkt. Chaula.

Akiwasilisha taarifa ya Huduma za Afya Tembezi, Mratibu wa huduma hiyo Dkt. Mombeki Domisian amesema tangu walipoanza kutoa huduma hii katika Mkoa wa Singida imeokoa maisha ya watanzania, imetoa elimu ya kinga, imepeleka utaalamu na zaidi imetoa ushauri kwa wagonjwa kulingana na ugonjwa husika.


Chanzo: Tovuti ya OR-TAMISEMI (www.tamisemi.go.tz)


Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.