Idara ya Afya ya Jiji la Dodoma imefanya kikao kilichojumuisha Waganga Wafawidhi wa Vituo vya Afya, Zahanati na Hospitali ili kukumbushana uwajibikaji, kutatua changamoto mbalimbali zinazoikumba sekta hiyo, kupitia mpango wa bajeti wa mwaka wa fedha unaotekelezwa sasa na kuanza kuandaa Mpango wa Bajeti wa mwaka wa fedha 2020/21.
Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Wilaya Daktari Gatete Mahava alipokuwa akitoa taarifa fupi ya kikao cha Idara yake kilichokaa Alhamisi ya tarehe 14/11/2019 katika ukumbi mkuu wa Mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Kikao hicho kimeshirikisha Waganga Wafawidhi kutoka Vituo vya Afya vinne (4), Zahanati (32) na Hospitali moja (1). Aidha, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) walialikwa kuhudhuria kikao hicho kama wadau muhimu wa utoaji wa huduma za Afya na kujadili masuala yanayozigusa taasisi hizi mbili katika utekelezaji wa majukumu yao.
Waganga Wafawidhi kutoka vituo vya Afya, Zahanati, na Hospitali wakiwa katika kikao cha tathmini ya utekelezaji wa majukumu yao na Mpango wa Bajeti wa mwaka 2020/21.
Wataalam wa huduma za Afya wakimsikiliza Mganga Mkuu wa Wilaya Daktari Gatete Mahava (hayupo pichani) wakati wa tathmini ya utekelezaji wa majukumu ya utoaji wa huduma za afya Jijini Dodoma.
Kikao cha Idara ya Afya kikiendelea.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.