• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Idara ya Mishahara yatakiwa kubuni njia za kutoa motisha kwa wafanyakazi

Imewekwa tarehe: March 11th, 2023

NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete ameitaka Idara ya Mishahara, Motisha na Marupurupu kubuni njia mbalimbali za kutoa motisha kwa watumishi wa umma ambazo zitatumiwa na waajiri Serikalini ili kuwajengea ari na morali ya kutoa huduma bora kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kutoa mchango katika maendeleo ya taifa.

Kikwete ametoa maelekezo hayo jijini Dodoma wakati wa kikao kazi chake na watumishi wa idara hiyo kilicholenga kufahamu majukumu yanayotekelezwa na kuhimiza uwajibikaji.

Kikwete amesema, zitafutwe njia nzuri na sahihi za kuwapa motisha watumishi wa umma ambazo hazitaathiri bajeti ya utekelezaji wa vipaumbele vya Serikali pamoja na miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa lengo la kuboresha miundombinu ya utoaji huduma muhimu kwa wananchi.

Kikwete amefafanua kuwa, motisha kwa watumishi wa umma si lazima iwe fedha bali inaweza kufanyika kwa kuboresha mazingira ya kazi kwa kuwapatia watumishi wa umma vitu mbalimbali kwa mfano bima ya afya ya uhakika itakayowawezesha kupata huduma bora ya matibabu na kuimarisha afya ili waendelee kuwahudumia wananchi ipasavyo.

“Motisha isijikite sana kwenye fedha, izingatie pia kuboresha mazingira ambayo yatamuwezesha mtumishi wa umma kutekeleza majukumu yake kikamilifu,” Mhe. Kikwete amesisitiza.

Kikwete ameongeza kuwa, yeye binafsi anaamini kwamba licha ya mtumishi wa umma kupata stahiki ya mshahara wake lakini motisha kwa mtumishi wa umma ni jambo muhimu sana katika kumuongezea ari, morali na ufanisi wa utendaji kazi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuujenga utumishi wa umma unaowajibika kwa wananchi kwa kutoa huduma bora, hivyo motisha kwa watumishi wa umma ni sehemu ya kulifikia lengo la kuujenga utumishi wa umma unaowajibika kwa umma.

Matangazo

  • Miaka miwili ya Rais, Dkt.Samia Suluhu Hassan March 19, 2023
  • Miaka miwili ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan March 19, 2023
  • Miaka miwili ya Rais, Dkt.Samia Suluhu Hassan March 19, 2023
  • Miaka miwili ya Rais, Dkt.Samia Suluhu Hassan March 19, 2023
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Maboresho makubwa sekta ya Afya Dodoma

    March 23, 2023
  • Miradi ya Mapato ya ndani yaanza kutoa matunda

    March 23, 2023
  • Agizo la Rais kuhusu Machinga latimia Dodoma

    March 22, 2023
  • Upatikanaji dawa, vifaa tiba waimarika

    March 21, 2023
  • Angalia zote

Video

Bwawa la Mtera kuhudumia Dodoma
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    3 CDA Street

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.