MGANGA Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Dkt. Gatete Mahava amekutana na viongozi wa Zahanati na vituo vya Afya kujadiliana utekelezaji wa shughuli mbalimbali zinazotolewa katika Jiji la Dodoma.
Akizungumza na wataalamu hao leo Novemba 25, 2020 katika ukumbi wa Jiji Dkt. Mahava amesema moja ya mambo ambayo wamejadiliana ni kuona kwa namna gani utekelezaji wa bajeti ya robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2020/2021 umefanywa.
“Kila kituo kilikuwa na bajeti yake kama mnavyo fahamu serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sasa hivi inapelekea fedha moja kwa moja kwenye vituo, na zile fedha zinazokwenda kule ni kulingana na bajeti zilizotengwa na kile kituo lazima sasa kama timu ya CHMT kuhakikisha kwamba tunafuatilia utekelezaji wa bajeti hizo’’
Kwa upande wake Sittu Muhunzi Muuguzii Mkuu Jiji la Dodoma amesema lengo kubwa ilikuwa ni kuongea na viongozi wa vituo vya afya ambao wanatoa huduma katika jiji la Dodoma ili kuona wametekeleza vipi majukumu yao ya kila siku.
“Tunataka kuona makusanyo ya vituo, yamekusanywa kiasi gani kulinga na malengo yao waliyokuwa wamejiwekea ndio leo tunajadili na wao watawasilisha mawasilisho ni kiasi gani wamefikia’’ alisema Sittu
Naye Maganga Mfawidhi wa kituo cha Chikande Ngaweji Nkinga amesema tayari wamepitia mwenendo wa wa utekelezaji wa bajeti na makusanyo ya vituo mbalimbali ambapo wamesisitizwa ili vituo vyao viweze kujiendesha ni lazima wawe na mpangilio mzuri wa ukusanyaji mapato.
“Tayari tumeshapitia mwenendo wa utekelezaji wa bajeti na kiongozi wetu ametusisitiza kwamba ili vituo viweze kujiendesha ni lazima kuwa na mpango mzuri wa ukusanyaji wa mapato na kama kuna mtu anachangamoto yeyote ile anatakuwa kuwasiliana na mganga mkuu wa jiji ambaye yuko kwa niaba ya mwajiri’’ Nkinga
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.