KATIBU Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Adolf Ndunguru amewaagiza walimu wakuu wa shule za msingi chini kuhakikisha wanaimarisha usimamizi wa ufundishaji na ujifunzaji kwa kuongeza ubunifu katika utatuzi wa changamoto za ujifunzaji kwa wanafunzi.
Ndunguru ametoa maagizo hayo jijini Mwanza wakati akifunga mafunzo kwa walimu wakuu na maafisa mazingira kuhusu miongozo ya ujenzi wa miundombinu ya shule, usalama wa mazingira na jamii na taratibu za ununuzi wa umma.
Amesema Serikali imeanza kutekeleza. itaala ya elimu iliyoboreshwa inayosisitiza utolewaji wa elimu itakayomwezesha mwanafunzi kupata ujuzi ili aweze kujitegemea na kuliletea Taifa maendeleo hivyo ni wajibu wa kila walimu kuhakikisha anatimiza majukumu yake kikamilifu.
Pia amewaelekeza walimu wakuu wote nchini kuhakikisha wanaweka mazingira wezeshi yatakayowasaidia walimu kushiriki kikamilifu Mafunzo Endelevu ya Walimu Kazini (MEWAKA) katika ngazi ya shule na vituo vya walimu ili kuboresha ufundishaji.
“Serikali imedhamiria kuboresha ufundishaji kupitia Mpango wa mafunzo endelevu kazini, hivyo nitumie fursa hii kuwaelekeza walimu wakuu wote nchini kwa kushirikiana na Wakurugenzi wa Halmashauri kuweka mazingira rafiki yatakayowawezesha walimu kushiriki kikamilifu katika MEWAKA na kuwapa usaidizi unaohitajika” amesema Ndunguru
Amesema kuwa uwepo wa mazingira salama na rafiki kunamuwezesha mwanafunzi kujifunza kwa ufasaha hivyo amewataka walimu hao kuweka mifumo na mikakati ya kuwalinda watoto dhidi ya unyanyasaji na ukatili wa aina yoyote.
Amewataka kuhakikisha klabu za wanafunzi zinahuishwa na wanafunzi kujengewa uwezo wa kujitambua, kujieleza, kujiamini na jamii ishirikishwe katika kuweka utaratibu wa kubaini na kushughulikia masuala ya ukatili, unyanyasaji na malalamiko.
Aidha, amewataka kuhakikisha wanasimamia ukamilishaji wa ujenzi wa miundombinu ya shule kwa wakati huku ujenzi huo ukiendana na thamani ya fedha iliyotolewa na Serikali ili kuweza kuleta manufaa kwa taifa na kutimiza vigezo vya kupata fedha
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.