WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, SelemaniJafo ameupongeza uongozi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma na Wakala wa Barabaramijini na Vijijini (TARURA) kwa ujenzi imara wa barabara Jamhuri na Msikiti waGadafi, yenye urefu wa kilomita 1,
Aidha, ametoa miezi 5 kukamilishwa kwa ujenzi wa barabara ya Nkuhungu-JCTChamwino yenye kilomita 1, inayokarabatiwa kwa kiwango cha lami nyepesi.
Jafo alitoa pongezi wiki iliyopita (tarehe 21/01/2021) jijini Dodoma marabaada ya kukagua ujenzi wa Barabara hizo.
Alisema ameridhishwa na ujezi wa barabara ya lami nzito uliotekelezwa naMkandarasi Nyanza Road kwa Gharama ya Sh bilioni 1.072 kwa muda wa siku 60,huku akihimiza kuimarisha usafi wa mitaro ya barabara hiyo.
“Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya mimi hapa sina wasiwasi kabisa, nimeridhika naujenzi huu na hasa ikizingatiwa kwamba eneo hili yanapita magari yenye uzitotofauti tofauti yakiwepo malori, hivyo kujenga kwa kiwango hiki cha laminzito ilikuwa ni sahihi kabisa”
Akiwa katika eneo la Barabara ya Nkuhungu- JCT Chamwino, Jafo, alitaka kujuamuda sahihi uliopangwa kukabidhi kazi hiyo ambayo imesita kwa muda kutokana nahali ya hewa.
Awali, Mhandisi wa TARURA Mkoa Lusako Kilembe, alimwambia Mhe. Waziri, kazihiyo inatazamiwa kukabidhiwa mwezi wa sita hatua iliyomlazimu Waziri kutoamaelekezo ya kuharakishwa kwa kazi.
“Mtendaji mkuu wa TARURA, huyu Mhandisi, msije mkamhamisha hapa anaonekanani mtu anayefahamu vema majukumu yake na hasa kwa mahitaji ya Makao Makuu yaNchi, nitoe rai tu, kufikia mwezi Juni kwa tarehe iliyopangwa kazi hii iweimekamilika."
Barabara ya Nkuhungu JCT Chamwino inajengwa kwa gharama ya Sh milioni 819.4,ambapo ujenzi wake unategemea kuchukua siku 180 hadi kumalizika.
Mhandisi Lusajo, aliahidi muda uliobakia ambao ni siku siku 140wakati maendeleo ya mradi huo umefikia asilimia 10 ya mradi mzima.
Akisoma taarifa ya ujenzi, Mhandisi wa TARURA, Mkoa wa Dodoma LusakoKilembe, alisema changamoto kubwa iliyoathiri mradi kutokamilika kwa wakati nimvua zinazoendelea kunyesha mfululizo mkoani hapo.
Barabara ya Nkuhungu JCT Chamwino, inajengwa na Mkandarasi G’s ContractorsCo. Ltd ya mkoani Iringa, ambapo urefu wa barabara ni Kilomita 1 inayojengwakwa kiwango cha lami nyepesi, ujenzi wa mifereji ya maji, mita 300 ujenzi wakalvat 8 na uwekaji wa alama za barabarani.
Waziri Jafo, alikuwa katika ziara za kukagua miradi mbalimbali ya maendeleoinayotekelezwa na wakala wa Barabara Mijini na Vijijini TARURA mjini Dodoma.
Chanzo: Tovuti ya TAMISEMI
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.