JAMII imehakikishiwa usalama, haki na usawa kwao na katika maeneo yao wakati ambao Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi utakapofanyika.
Hayo yalisemwa leo na Afisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi kutoka Wizara ya Ardhi Tumaini Setumbi Jijini Dodoma ambapo Wizara huyo imeendesha mafunzo kwa kamati za Urasimishaji kwa Mitaa ya Bihawana, Mapinduzi A na B pamoja na Mpunguzi.
Setumbi alisema kuwa Mradi huo utahakikisha haki zinasimamiwa kwa makundi yote maalumu ya kinamama, wazee, watoto na watu wenye ulemavu ili waweze kupata haki zao za umiliki wa Ardhi sawa na watu wengine.
“Idadi ya wanawake wanaomiliki Ardhi ni ndogo ukilinganisha na Wanaume hivyo moja kati ya kazi yetu ni kuielimisha jamii kuwa wanawake pia wanayo haki sawa na wanaume kumiliki Ardhi” aliongeza Setumbi.
Mradi huo ni jitihada za Serikali kuhakikisha kwamba migogoro ya Ardhi inapungua na Wananchi wanapata hati miliki ambapo imetenga zaidi ya Bilioni 345 ukiwa na lengo la kuimarisha miundombinu itakayorahisisha huduma za ardhi nchini.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.