JAMII imeshauriwa kufanya mazoezi mbalimbali ya mwili ili kuepuka kuugua magonjwa yasiyo ya kuambukiza na gharama kubwa za matibabu.
Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza katika hotuba yake ya kufungua tamasha la michezo katika wiki ya kupinga magonjwa yasiyoambukiza inayofanyika kitaifa katika uwanja wa michezo wa Jamhuri jijini Dodoma leo.
Shonza amesema “napenda kutoa wito kwa wananchi wote kushiriki kufanya mazoezi ya mwili. Mazoezi ni muhimu kwa afya kwa sababu yatasaidia kuepuka magonjwa yasiyoambukiza na kuipunguzia serikali mzigo wa kugharamania matibabu”. Aidha, ameshauri kuwa tamasha la michezo la wiki ya kupinga magonjwa yasiyoambukiza litumike kufanya tathmini ya mfumo wa maisha ili kupunguza hatari ya kupata magonjwa hayo.
Sonza amekazia kuwa mazoezi mazuri ni yale yanayofanyika angalau kuanzia dakika 30 na kuendelea. Vilevile, alishauri kuwa jamii iwe inafanya mazoezi siku zisizopungua tatu kwa wiki.
Tamasha la michezo la kuhamasisha wananchi kupambana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza kitaifa lilitanguliwa na mbio za marathoni zilizoshirikisha wanariadha kutoka ndani na nje ya nchi.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.