MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele, amezindua Mitambo ya kuzalisha zege ‘Concrete Bunching Plants, Concrete Truck Mixer pamoja na Concrete pump, itakayotumiwa na SUMAJKT Construction Company Limited’ eneo la Mwangaza Jijini Dodoma.
Akitoa hotuba wakati wa Uzinduzi, Mkuu wa JKT ambae pia ndie Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT, ameipongeza Menejimenti ya Shirika pamoja na Uongozi wote wa SUMAJKT Construction Company Limited, kwa uamuzi wa kununua mitambo hiyo ambayo kwa kiasi kikubwa itarahisisha utendaji kazi pamoja na kuongeza tija.
Aidha, Meja Jenerali Mabele, aliishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais na Amiri Jeshi Mkuu, kwa kuendelea kuiamini JKT kwa kuipatia miradi mbalimbali ya Serikali.
Akihitimisha Hotuba yake, Mkuu wa JKT, aliwataka watendaji wote watakaokabidhiwa kuendesha Mitambo hiyo, kuitunza na matengengenezo (service) yake iwe inafanyika kwa wakati ili ilete tija inayokusudiwa.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi ya SUMAJKT, Meja Jenerali Farah Mohamed (Mstaafu), amepongeza ununuzi wa Mitambo hiyo mipya na ya kisasa kwamba itaongeza thamani katika Shirika kwa kuwa na ubora wa bidhaa zitakazo zalishwa, urahisi wa upatikanaji wake, gharama za uzalishaji zitapungua na pia muda wa uzalishaji utapungua kuliko ilivyokuwa hapo awali.
Naye Mkurugenzi wa SUMAJKT, Kanali Petro Ngata, amewapongeza watendaji wote kwa ushirikiano ili kuhakikisha Shirika linafikia malengo ya ukuaji, kuongeza mapato na kujenga uwezo wa Shirika kuendelea kuwekeza katika miradi mipya na vitendea kazi.
Akielezea matumizi ya Mitambo hiyo, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Ujenzi ya SUMAJKT CONSTRUCTION COMPANY LIMITED, Injinia Morgan Nyoni, amesema baada ya kupokea Mitambo hiyo, tayari usimikwaji umekamilika na uwepo wake utaongeza kipato kwa Kampuni ya Ujenzi na Shirika kwa ujumla kwa kuwa hitajio la zege Jijini Dodoma ni kubwa na itaongeza imani kiutendaji kutoka kwa washitiri.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.