Na. Dennis Gondwe, DODOMA
HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imejipanga kujenga na kukamilisha makao makuu yake katika mwaka wa fedha 2023/2024 ili kuweza kutoa huduma bora kwa wananchi.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru alipokuwa akifafanua vipaumbele vya Mpango na Bajeti ya Halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Mafuru alisema kipaumbele namba tatu ni ujenzi wa makao makuu. “Halmashauri ya Jiji la Dodoma kila bajeti lazima kuwe na mradi mkubwa wa maendeleo kwa maana ya uwekezaji. Safari hii tunakwenda kufanya uwekezaji kwenye ukamilishaji wa ujenzi wa makao makuu ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Katika bajeti hii ujenzi utaanza ambapo tunajenga pale Nzuguni. Tunajenga ofisi kubwa na nzuri na chini kitega uchumi na juu ofisi” alisema Mafuru.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.