HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imefanikiwa kutekeleza uboreshaji wa makazi yaliyokuwa holela kwa asilimia 80 na kuwahakikishia wananchi maisha bora.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa Mipango Miji wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Aisha Masanja alipokuwa akiwasilisha mada juu ya uboreshaji wa makazi ndani ya Jiji la Dodoma katika Maadhimisho ya Siku ya Makazi Duniani yaliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu jijini Dodoma.
Masanja alisema kuwa Halmashauri imefanikiwa kutekeleza kwa asilimia 80 uboreshaji wa makazi yaliyokuwa holela ndani ya Jiji la Dodoma pamoja na kupanga makazi mapya. “Tunahakikisha kila kipande cha ardhi ndani ya Jiji la Dodoma kinapangwa na kupimwa ili kulinda Jiji kwa sasa na miaka ijayo kwa mipango endelevu ya matumizi ya ardhi, kuhifadhi ardhi na kuboresha makazi kwa kila mkazi wa dodoma na nchi kwa ujumla”
Afisa Mipango Miji wa Jiji la Dodoma, Aisha Masanja (wa kwanza kulia) akiwa meza kuu pamoja na viongozi na watoa mada wengine kwenye Maadhimisho ya Siku ya Makazi Duniani iliyofanyika Jijini Dodoma katika Ukumbi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.