HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imefanikiwa kutoa hati za umiliki ardhi 5,000 kwa mwaka wa fedha 2018/2019 na kushika nafasi ya kwanza nchini katika utoaji hati nyingi.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi alipokuwa akikabidhi barua za viwanja 144 kwa wananchi ambao ardhi yao ilitwaliwa na serikali wakati wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) katika ukumbi Halmashauri ya Jiji.
Kunambi alisema kuwa Halmashauri ya Jiji imetoa hati 5,000 za umiliki ardhi. “Kwa Tanzania Halmashauri ya Jiji tunaongoza kwa kutoa hati nyingi, tukifuatiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela iliyotoa hati 2,000. Na Waziri wa Ardhi alitoa taarifa hiyo bungeni” alisema Kunambi.
Akiongelea zoezi la ugawaji viwanja 144 kwa wananchi wa Mtaa wa Sechelela Kata ta Tambukareli ambao ardhi yao ilitwaliwa na iliyokuwa CDA, alisema “leo hii wananchi 144 nimewapa viwanja bure, kwa maana wanalipa zile gharama za kawaida za kisheria takribani shilingi 700,000 badala ya shilingi 7,000,000. Hii ni heshima kubwa kwa Mheshimiwa Rais ambaye siku zote amekuwa akipambana kuwakomboa wananchi wanyonge. Sisi wasaidizi wake tunaimba na tunacheza wimbo huo”.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.