• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Jiji Dodoma laongoza maonesho ya Nanenane

Imewekwa tarehe: August 8th, 2020

HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imeendelea kushika nafasi ya kwanza katika maonesho ya Nanenane Kanda ya Kati kwa Halmashauri zote za Mkoa wa Dodoma kutokana na ushirikiano wa kitaasisi na wadau wengine katika kufikisha teknolojia kwa wananchi.

Akiongea wakati wa kutoa zawadi kwa washindi, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia watu wenye ulemavu, Stella Ikupa aliyemuwakilisha mgeni rasmi Waziri wa Sheria na Katiba, Mwigulu Nchemba aliwapongeza washindi.

Ikupa alisema “niwashukuru na kuwapongeza sana washindi wote kutokana na kazi nzuri mliyoifanya hadi kupata ushindi huu”. Aidha, aliwataka kuendelea kuwa mfano mzuri katika sekta za kilimo, mifugo na uvuvi ili kuwawezesha wananchi kukua kiuchumi.

Halmashauri ya Jiji la Dodoma imeibuka mshindi ikizishinda Halmashauri saba za Mkoa wa Dodoma katika eneo la maonesho ya mabanda kwa Halmashauri.

Akiongelea ushindi huo, Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA na Uhusiano katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Fungo alisema kuwa ushindi huo ni kielelezo cha dhamira thabiti ya Halmashauri kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi wa Jiji hilo ili kuwasaidia kukuza uchumi. “Halmashauri ya Jiji baada ya kupewa hadhi ya kuwa Jiji na Mheshimiwa Rais, Dkt. John Magufuli, vijiji vyote vimefutwa na hivi sasa Jiji lina mitaa 222. Hivyo, basi tumejipanga kuhakikisha katika Jiji la Dodoma tunafanya kilimo cha mjini. Katika Mpango Kabambe (Master Plan) wa Jiji, yametengwa maeneo maalum kwa ajili ya kilimo cha mjini. Kwa muktadha huo, Jiji limekuwa na mkakati wa kuhakikisha linatoa elimu ya kilimo, na ufugaji wa kisasa kwa kutumia teknolojia za kisasa. Hiki ndicho tumefanya katika maonesho ya 27 ya Nanenane mwaka huu na ushindi wetu ni uthibitisho kuwa mikakati ya lengo letu imeanza vizuri” alisema Fungo.

Akiongelea maonesho hayo, alisema kuwa Halmashauri hiyo ilionesha teknolojia za umwagiliaji kwa kutumia miundombinu ya umwagiliaji wa matone, usindikaji na uhifadhi wa bidhaa kwa kutumia vifungashio vyenye ubora na mbinu za ufugaji wa kisasa na uandaaji wa malisho ya mifugo. Maeneo mengine aliyataja kuwa ni ufugaji samaki wa kisasa na nyuki.

Vilevile, kulikuwa na maonesho ya kilimo cha mbogamboga, matunda na mazao ya nafaka kwa kutumia mbinu za kisasa, aliongeza.

Fungo alitoa wito kwa wananchi wa Jiji hilo kuendelea kutumia fursa hiyo adhimu ya kupata mbinu za kilimo na ufugaji wa kisasa katika mazingira ya Jiji. “Jiji linao wataalam wa kutosha na katika banda letu hapa Nanenane tutaendelea kuonesha na kufundisha mbinu hizo kwa muda wote kama ilivyoagizwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Mheshimiwa Selemani Jafo.

Katika maonesho ya 27 ya Nanenane Halmashauri ya Jiji la Dodoma ilishika nafasi ya kwanza ikiwa ni mwaka wa pili mfululizo, Halmshauri ya Wilaya ya Kondoa ilishika nafasi ya pili na Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa nafasi ya tatu, washindi wote walizawadiwa vyeti.

Wataalam wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya kupokea cheti ya ushindi wa kwanza kwa Halmashauri za Mkoa wa Dodoma kwenye maonesho ya 27 ya Nanenane yaliyofanyika katika uwanja wa Nanenane Nzuguni Jijini Dodoma.

Mgeni rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (watu wenye ulemavu), Stella Ikupa akimkabidhi cheti cha ushindi wa kwanza kwa Halmashauri zote za Mkoa wa Dodoma, Katibu Tawama Wilaya ya Dodoma Mjini, Michel Maganga akipokea cheti ya ushiri wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika maonesho ya 27 ya Nanenane jijini Dodoma.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma atoa pongezi kwa Madiwani

    May 25, 2025
  • Mkopo wa 10% tija kwa maendeleo ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu

    May 23, 2025
  • Mkopo wa 10% tija kwa maendeleo ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu

    May 23, 2025
  • Wananchi Kata ya Madukani washukuru kuboreshwa huduma za Afya, Zahanati ya Chikande

    May 21, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.