Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa mara nyingine tena imeongoza kwa ukusanyaji wa Mapato ya ndani kwa kukusanya mapato ghafi zaidi ya Halmashauri zote nchini.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mitaa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo alipokuwa akitoa tathmini ya ukusanyaji mapato kwa Halmashauri zote nchini kwa mwaka wa fedha 2018/19.
Aidha, kwa mara ya kwanza Nchini Halmashauri zote 185 zimefanikiwa kukusanya sh. bilioni 661.4 ambayo ni sawa na asilimia 91 ya malengo ya mwaka wa Fedha 2018/19 ya kukusanya sh bilioni 723.
Matokeo haya ni ongezeko la asilimia 9 kwa Mwaka wa Fedha 2018/19 ukilinganisha na makusanyo ya asilimia 81 ya Mwaka wa Fedha 2017/18 huku Halmashauri ya Jiji la Dodoma sambamba na Mkoa wa Dar es salaam zikiongoza kwa mapato ghafi.
Hayo yabamebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa alipokuwa akitoa taarifa ya mapato na matumizi ya fedha za vyanzo vya ndani vya halmashauri kwa mwaka wa fedha 2018/19. Mapato haya ya ndani hayajumuishi vyanzo vinavyokusanywa na Serikali kuu.
Akifafanua zaidi Mhe. Jafo alisema halmashauri za Wilaya tano zilizoongoza kwa kigezo cha asilimia ya mapato ya ndani kuwa ni Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi (asilimia 171), Wanging’ombe (asilimia 165), Kilolo (asilimia 150), Misenyi (asilimia 142) huku Mbeya DC ikishika nafasi ya tano kwa kukusanya asilimia 141.
Halmashauri za Wilaya zilizofanya vibaya kiasilimia ni Tandahimba DC (asilimia 19), Msalala (asilimia 19), Masasi DC (asilimia 26) Newala (asilimia 27) pamoja na Nanyumbu (asilimia 36).
Kwa kigezo cha pato ghafi, Mhe. Jafo alisema "halmashauri zilizoongoza kwa wingi wa mapato kuwa ni Halmashauri ya Jiji la Dodoma (Sh bilioni 71.7), Ilala (Sh bilioni 58.1), Kinondoni (Sh bilioni 34) Temeke Sh bilioni 33.3), Ubungo (bilioni 18.6) na Jiji la Arusha (Sh bilioni 16.4) wakati halmashauri tano zilizofanya vibaya katika kundi hili ni Nanyamba (sh milioni 258), Gairo DC(Sh milioni 396), Kigoma DC (Sh milioni 397.1) Buhigwe (Sh milioni 403.8) na Kakonko DC (Sh milioni 403.8)".
Vilevile, katika kundi la mikoa kwa kigezo cha asilimia, Jafo alisema mikoa inayoongoza kwa kigezo cha asilimia ya mapato ya ndani ni Mkoa wa Geita (asilimia 119), Iringa (asilimia 117), Songwe (asilimia 112), Kagera (asilimia 105) na Njombe (asilimia 104), wakati mikoa iliyofanya vibaya katika kundi hili ni Mtwara (asilimia 42), Simiyu (asilimia 45.9), Shinyinga (asilimia 62), Kigoma (asilimia 74) Mara na Morogoro (asilimia 80).
Kwa upande wa mikoa kwa kigezo cha pato ghafi, Mhe. Jafo alitaja Mikoa inayoongoza kuwa ni Dar es Salaam (Sh bilioni1 163.5), Dodoma (Sh bilioni 82.6), Mwanza (Sh bilioni 32.6) Arusha (Sh bilioni 31.9) na Mbeya (Sh bilioni 31.4) wakati mikoa iliyofanya vibaya katika kundi hili ni Katavi (Sh bilioni 7.3), Kigoma (Sh bilioni 7.7), Rukwa (Sh bilioni 8.2) Simiyu (Sh bilioni 8.8) na Njombe (Sh bilioni 11.4).
Tena, Jafo alisema Jiji la Arusha limeongoza katika kundi la halmashauri za majiji kwa asilimia kwa kukusanya asilimia 105 ya makisio huku jiji la Mbeya likiwa la mwisho katika kundi hilo baada ya kukusanya asilimia 89 ya makisio.
Alisema Halmashauri ya Jiji la Dodoma inaongoza kwa kigezo cha pato ghafi ambapo imekusanya Sh bilioni 71.7 na halmashauri ya jiji la Mbeya imekuwa ya mwisho baada ya kukusanya Sh bilioni 11.4.
Zaid ya hayo, Jafo alisema halmashauri ya manispaa ya Sumbawanga imeongoza kundi la halmashauri za Manispaa kwa kukusanya asilimia 138 ya makisio huku Lindi ikishika nafasi ya mwisho kwa kukusanya asilimia 54 ya makisio.
Jafo alisema kwa upande wa halmashauri ya Manispaa ya Ilala imeoongoza katika kundi la halmashauri za Manispaa kwa kigezo cha mapato ghafi baada ya kukusanyw Sh bilioni 58 huku Lindi ikiwa ya mwisho kwa kukusanya Sh bilioni 1.0.
Aidha, Jafo alisema halmashauri ya Mji wa Geita imeongoza kundi la halmashauri za miji kwa kigezo cha asilimia ambapo wamekusanya kwa asilimia 157 ya makisio huku halmashauri ya Mji wa Nanyamba imekuwa ya mwisho baada ya kukusanya asilimi 11 ya makisio.
“Katika kigezo ya pato ghafi kwa halmashauri za mji, Geita inaongeza baada ya kukusanya Sh bilioni 8.02 na halmashauri ya mji wa Nanyamba imekuwa ya mwisho ikiwa imekusanya Shilingi milioni 257.6.
Kwa upande wa halmashauri za wilaya, Jafo alisema Mbozi inaongoza kwa kukusanya kwa asilimia 171 ya makisio na ya mwisho ni Tandahimba iliyokusanya asilimia 19 ya makisio wakati kwa upande wa pato ghafi, Chalinze inaoongoza kwa kukusanya Sh bilioni 7.6 na ya mwisho katika kundi hili ni Gairo iliyokusanya Sh milioni 396.1.
Vilevile, Jafo aliwataka wakurugenzi ambao Halmashauri zao zimefanya vibaya katika ukusanyaji wa mapato kujitathimini na kuweka mikakati ya kuongeza vyanzo vya mapato na mapato ya halmashauri zao kwa ujumla.
Pia Waziri Jafo aliwaagiza Wakurugenzi ambao Halmashauri zao zimetoa mikopo ya wanawake, vijana na walemavu chini ya asilimia 50 kuandika barua za maelezo kwanini wasichukuliwe hatua kwa kuvunja sheria na barua hizo ziwasilishwe ndani ya muda wa wiki mbili.
Aliongeza kuwa Wakurugenzi wote wahakikishe ukusanyaji wa mapato hayo ya ndani unaenda sambamba na upelekaji wa fedha kwenye miradi ya maendeleo na mikopo kwa wanawake, vijana na walemavu.
Hata hivyo, Mhe. Jafo ameendelea kusisitiza matumizi ya mifumo ya kielektroniki katika ukusanyaji wa mapato ya ndani ili kuzuia upotevu wa mapato hayo.
Chanzo: tovuti ya tamisemi : (www.tamisemi.go.tz)
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.