HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma ilitoa shilingi 72,000,000 kutoka mapato yake ya ndani kwa ajili ya ukarabati wa majengo katika kituo cha Afya Makole kilichopo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Akiongea mbele ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi alisema kuwa Halmashauri ilitoa shilingi 72,688,056 kutoka katika mapato yake ya ndani kukarabati majengo ya kituo cha Afya Makole kutokana na kuwa yamechakaa.
Kunambi alisema kuwa fedha hizo zilitolewa kwa ajili ya ukarabati wa majengo ya zamani, ujenzi wa njia ya watembea kwa miguu, uzio wa nyumba ya mtumishi na sehemu ya kukaa wateja kwenye maabara mpya.
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Makole, Dkt. George Matiko alisema kuwa ukarabati huo umekiongezea kituo hicho uwezo wa kutoa huduma bora kwa wananchi.
Yustina Vicent, ambaye ni mgonjwa aliyeenda kupata huduma katika kituo hicho, alisema huduma zimeboreshwa mno kwa miaka miwili iliyopita.
Kituo cha Afya Makole kilianzishwa mwaka 1978 kikiwa ni moja ya vituo vinne vya Afya vya Serikali vilivyopo katika Jiji la Dodoma.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.