OFISI ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Dodoma kwa kushirikiana na Halmashauri ya Jiji la Dodoma wametoa elimu kwa wamiliki wa ardhi kuhusu ujenzi bila vibali ili kuepuka usumbufu wakati wa ujenzi.
Lengo la kampeni hiyo ni kuwafikishia mwananchi hususani wa jiji hilo elimu kuhusu umiliki wa ardhi, ujenzi kwa kufuata taratibu za mipango miji kodi ya pango la ardhi na fursa mbalimbali.
Afisa Habari wa Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Dodoma Hassan Mabuye amesema kampeni hiyo kwa awamu ya kwanza itafanyika siku tano mfululizo na inatajiwa kukamilika Jumatatu kesho.
Mabuye amesema zoezi la kuwafuata wananchi katika maeneo yao na kuwapatia elimu hiyo kuhusu masuala mbalimbali ya ardhi ni endelevu na hapo baadaye itafanyika katika wilaya zote za mkoa wa Dodoma.
"Mpaka sasa tumeshazunguka na kutoa elimu hii katika maeneo kadhaa ya jiji la Dodoma kama Ihumwa, Nzuguni, Chang'ombe, Nkuhungu, Majengo, Mnadani Swaswa, Ilazo, Kikuyu, Chidachi, Makulu na Mnada wa Kizota na muitikio ni mkubwa sana,” amesema Mabuye.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.