HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma inafanya oparesheni ya kawaida ya kukagua vyanzo vya mapato ikiwa ni pamoja na kukusanya kodi kwa wafanyabiashara Jijini hapa, ili kuweza kufikia malengo na bajeti waliyojiwekea katika kuelekea mwishoni mwa mwaka wa fedha wa 2020/2021.
Akizungumza na mwandishi wetu Mhasibu wa Kitengo cha Mapato wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Mafita Omary amesema kuwa mapato hayo ndiyo yanayomuwezesha Mkurugenzi kutoa huduma mbalimbali kwa Wananchi zikiwemo za Elimu na Afya.
Aidha, Omary aliongeza kuwa oparesheni hiyo itagusa katika vyanzo vyote vya mapato vya Halmashauri hiyo ikiwa ni pamoja na kukusanya ushuru wa huduma (City service levy), leseni za biashara, ushuru wa masoko, kodi za pango kwenye vizimba pamoja na ushuru wa hoteli.
“Ili ni zoezi la kawaida ambalo tunalifanya kila siku isipokua tumeamua kuongeza nguvu tunapoelekea mwisho wa mwaka wa fedha wa 2020/2021 ili tuweze kufikia lile lengo au bajeti ambayo tulijiwekea wenyewe katika ustawi wa Halmashauri yetu” Alisema Omary.
Alitoa wito kwa wakazi wa Jiji la Dodoma kutoa ushirikiano kwa timu hiyo itakapokua inapita katika maeneo yao ya biashara pamoja na kuwakumbusha wale wote ambao hawajalipa ushuru au wamelipa nusu kufika katika ofisi za Jiji kwa ajili ya kufanya malipo huku akiwataka wafanyabishara wasio na leseni kukata leseni mara moja ili kuepusha usumbufu.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.