HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma kuendesha mnada wa hadhara na upangishaji eneo la Bustani ya Mapumziko Chinangali (Chinangali Recreational Park) katikati ya Jiji la Dodoma.
Katika tangazo lililotolewa katika tovuti ya Halmashauri hiyo na kupatikana katika mbao za matangazo na mitandao ya kijamii linasomeka kuwa mnada huo utafanyika tarehe 14 Juni, 2020 saa 5.00 asubuhi katika Bustani ya Mapumziko Chinangali. Tangazo hilo linautaja mnada huo kuwa wa wazi kwa wananchi na wafanyabiashara wote.
Bustani hiyo inasifika kwa kuwa na mabwawa ya kisasa ya kuogelea Watoto na wakubwa, sehemu ya michezo mbalimbali ya watoto, jukwaa kubwa la sanaa. Maeneo mengine ya mvuto ni viwanja vya michezo ya tenisi, mpira wa kikapu, wavu na eneo la mazoezi ya mwili (gym). Tangazo hilo linaendelea kutaja maeneo ya kuuzia vyakula na vinywaji pamoja na nafasi ya kutosha ya maegesho ya magari.
Ikumbukwe kuwa Bustani ya Mapumziko Chinangali ina eneo la ukubwa wa ekari 12.3 na njia za kutembea ndani ya bustani zenye urefu wa kilometa 1.25, eneo hilo lina uwezo wa kuuegesha magari zaidi ya 100 kwa wakati mmoja.
Moja ya sehemu za michezo ya watoto
Jukwaa la michezo ya sanaa na utamaduni
Bwawa la kuogelea la wakubwa
Vibanda kuwa ajili ya vinywaji, snaks na nyama choma.
Pambo la mnala wa maji yanayoruka.
Mandhari nzuri ya kuvutia yenye sanamu za wanyama pori mbali mbali ndani ya eneo la mapumziko.
Mwonekano wa Eneo la Mapumziko la Chinangali kutoka angani.
Vibanda vya vinywaji, nyama choma, nk.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.