Na. Dennis Gondwe, DODOMA
HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma kutekeleza agizo la Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango la kupanda miti kwa kutumia njia ya mkataba ili kupima matokeo.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru alipokuwa akimkaribisha mwenyekiti wa mkutano maalum wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dodoma lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo kupitia rasimu ya Mpango na Bajeti kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Mafuru alisema kuwa Makamu wa Rais aliagiza miti ipandwe katika maeneo ya taasisi na maeneo mbalimbali. “Tunakwenda kutekeleza agizo la Makamu wa Rais la kupanda miti kwa mikataba. Walimu wa msingi, walimu wa sekondari na madaktari tunakwenda kwa kusainiana mikataba. Mfano tukisema kituo cha Afya Hombolo tunapanda miti 20, tunaandikishana na daktari na tunasaini mtakaba na tunapima matokeo. Haya mambo ya kupanda miti mvua zikiisha tunapoteana imefika mwisho” alisema Mafuru.
Akiongelea nafasi ya waratibu elimu kata, mkurugenzi aliwataja kuwa wana umuhimu mkubwa katika kuleta mabadiliko ndani ya jiji la Dodoma. “Waratibu elimu kata, hawa watu wanaelea, lakini serikali inawagharamia sana. Awamu hii tunakabana kwenye matokeo, tunakabana kwenye ujenzi na tunakabana kwenye miti. Pia tutakwenda nao kwa mikataba ili mwisho wa siku tuhojiane utekelezaji” alisema Mafuru.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.