HALMASHAURI ya Jiji la limetoa shilingi milioni 600 kwa vikundi vya Wajasiriamali Wanawake, Vijana, na Walemavu ili wajiimarishe katika shughuli zao za kiuchumi, huku ikitarajia kutenga zaidi ya Bilioni 4 kwa ajili ya vikundi hivyo katika mwaka ujao wa Fedha.
Kabla ya kukabidhiwa fedha hizo, wajumbe wa vikundi mbalimbali zaidi ya 100 vya Wajasiriamali hao wamepatiwa semina elekezi ya jinsi ya kutumia fedha hizo kwa malengo yaliyokusudiwa ili waweze kutengeneza faida na kurejesha mikopo hiyo na kuwezesha wanafaika wengine kukopeshwa.
Akifungua semina elekezi hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Dodoma jana, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Hidaya Maeda aliwakumbusha Wajasiriamali hao juu ya umuhimu wa kutumia mikopo kwa malengo mahsusi yaliyokusudiwa na kufanya marejesho kwa wakati ili Halmashauri ikopeshe wahitaji wengine.
“kwa upande wa Wanawake kumekuwa na mwendelezo mzuri wa kufanya marejesho ya mikopo, changamoto ni kwa vijana…wamekuwa hawafanyi vizuri katika kurejesha” alisema Maeda wakati akizungumza na wanavikundi hao.
Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Fedha na Biashara wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Alferd Mlowe aliwashauri Wajariamali hao kuwa na nidhamu katika matumizi ya Fedha wanazokopeshwa ili waweze kukuza mitaji yao kwa haraka na kuwa Wajasiriamali wakubwa nchini.
Alisema kwa mwaka ujao wa Fedha, Halmashauri ya Jiji la Dodoma inatarajia kutenga zaidi ya Shilingi Bilioni 4 kwa ajili kukopesha vikundi vya Wajasiriamali.
“Tusifikirie Fedha mnazokopeshwa na Halmshauri ni kama zawadi, hasa vijana msitumie Fedha hizo vibaya…tuzitumie kwa malengo na mikakati mliyojiwekea katika vikundi vyenu” alisisitiza.
Kwa mwaka huu wa Fedha, Halmashauri ya Jiji la Dodoma inatarajia kutoa mikopo ya zaidi ya Shilingi Bilioni 2.6 kwa vikundi hivyo.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Wajasiriamali hao Hudson Seme aliishukuru Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kuwa na mikakati endelevu y kuendeleza Wananchi kiuchumi huku akitoa wito kwa Wajasiriamali hao kukuza mitaji yao na kujiendesha wenyewe badala ya kutegemea misaada kila wakati kwani wahitaji ni wengi.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.