HALMSHAURI ya Jiji la Dodoma inatarajia kujiendesha kwa kujitegemea kwa asilimia mia ifikapo mwaka 2022, ikiwa ni pamoja na kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kutumia makusanyo yake ya ndani.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Godwin Kunambi wakati akiwasilisha taarifa katika mkutano mkuu wa ALAT Taifa unaofanyika Jijini Dodoma jana.
Alisema Halmashauri ya Jiji la Dodoma inalenga kufikia makusanyo ya kodi yapatayo bilioni 150 kutoka katika vyanzo vyake vya ndani hali itakayoiwezesha kulipa mishahara ya wafanyakazi wake wote na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.
“Kwa mwaka wa fedha huu tulionao sasa, Serikali Kuu inatuletea bilioni 53 tu…kwa maana ya bilioni 47 kwa ajili ya mishahara na bilioni tano za miradi ya maendeleo, na malengo yetu ni kukusanya bilioni 150” alifafanua Kunambi.
Alisema Halmashauri ya Jiji hilo imejipanga kuwa na vyanzo endelevu vya mapato ya ndani, huku akitaja mambo matatu yanayoweza kuzivusha Halmashauri zetu nchini kuwa ni pamoja na uzalendo, kujitoa, na kubadili fikra kwa kuamini kuwa kila kitu kinawezekana.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.