• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Jiji kupeleka timu ya maafisa mazingira na afya kukagua usafi Ipagala

Imewekwa tarehe: July 22nd, 2023

Na. Dennis Gondwe, IPAGALA

HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma kupeleka timu ya maafisa mazingira na afya kufanya ukaguzi katika maeneo ya Mtaa wa Ipagala kukagua hali ya usafi wa mazingira kutokana na changamoto wa baadhi ya wakazi wa maeneo hayo kutojitokeza kufanya usafi wa mazingira.

Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Kitengo cha Usafi na uthibiti wa taka ngumu Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dickson Kimaro alipokuwa akiongea na mamia ya wakazi wa Kata ya Ipagala waliojitokeza katika usafi wa pamoja kwenye korongo la kitaa cheusi.

Kimaro alisema “kwa sababu eneo hili lina changamoto ya wananchi kutojitokeza kufanya usafi katika maeneo yao. Wananchi wanalalamika kuwa watu wanaokaa kwenye nyumba zenye mageti hawajitokezi kufanya usafi na kuwaanchia wanaoishi katika nyumba zisizo na mageti kufanya usafi. Nimetoa maelekezo kwamba wiki ijayo kuanzia siku ya Jumatatu timu ya maafisa afya na mazingira watapita nyumba kwa nyumba kuhamasisha usafi na ambao watakaidi tutachukua hatua kwa mujibu wa sheria”.

Akiongelea zoezi la usafi wa pamoja, alisema kuwa usafi wa pamoja ulifanyika katika Kata ya Ipagala na Kizota. “Kwa wiki hizi mbili tumeweka nguvu zaidi na kushiriki sisi wenyewe viongozi kwa Kata ya Ipagala na Kizota ambapo tulibaini kuna baadhi ya maeneo ambayo ni machafu na wananchi hawajitokezi kufanya usafi. Leo tumekuwa katika eneo la Sulungai na Ipagala katika Korongo la Kitaa cheusi. Tumegundua wananchi wanatupa taka ovyo na tumekuta wananchi wanatupa hata pampasi” alisema Kimaro.

Alisema kuwa kuna wakati vikundi vya kijamii ambavyo vimepewa jukumu la kukusanya taka nao wanazitupa katika korongo hilo. “Tumehamasisha wananchi na kujitokeza kufanya usafi katika korongo hili na wiki iliyopita tulifanya usafi eneo hilo. Tumetoa maelekezo kwa wananchi wote kujiepusha na tabia ya kutupa taka ovyo kwasababu usafi ni ustaarabu na unaanza na sisi wenyewe” alisema Kimaro.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Ipagala, Elenei Mogwa aliwashukuru wananchi waliojitokeza kushiriki zoezi la usafi wa mazingira. “Zoezi la usafi wa mazingira katika korongo hili ni zoezi endelevu mpaka korongo letu litakapokuwa safi. Mnapowaona viongozi wa halmashauri tupo nao hapa njue ni viongozi waliokuja kukagua usafi na kusimamia sheria. Hatua zikianza kuchukuliwa kwa wale ambao hawatekelezi maelekezo ya usafi wa mazingira mjue ni utekelezaji wa maelekezo rasmi kwa mujibu wa sheria” alisema Mogwa.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.