HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imejipanga kuhakikisha inatokomeza changamoto ya upungufu wa madawati Jijini hapa ndani ya mwaka huu wa 2021.
Hayo yamesemwa na Afisa Elimu Vifaa na Takwimu Idara ya Elimu Sekondari Mwalimu Fredrick Mwakisambwe (pichani juu) alipotembelea katika karakana ya Jiji ya utengenezaji wa madawati hayo.
Mwl. Mwakisambwe amesema kuwa mpango huo ulianza mwezi wa kwanza mwaka 2021 ambapo mpaka sasa jumla ya madawati 3,090 yamekwisha tengenezwa huku madawati 590 yakiwa ni kwa upande wa shule za msingi na 2,500 kwa shule za sekondari.
"Lengo la Halmashauri ni kutengeneza jumla ya madawati 6,000 ifikapo mwisho wa mwaka huu, ambapo kati ya hayo madawati 1,000 yatakwenda kwenye shule za msingi na 5,000 kwa shule za sekondari" amesema Mwl. Mwakisambwe.
Aidha, amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri kwa kuipa kipaumbele Idara ya Elimu jambo ambalo linachangia kwa kiasi kikubwa kuinua sekta ya hiyo Jijini hapa.
Fundi wa karakana ya madawati ya Jiji la Dodoma akipanga moja ya meza ambazo zimekwisha kamilika.
Madawati pamoja na vifaa vinavyotumika kutengeneza madawati.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.