Usafi wa Mazingira Jumamosi hii umefanyika katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dodoma. Katika Kata ya Miyuji usafi ulifanyika katika eneo la Makaburi ya Wahanga ambapo pia kuliambatana na zoezi la upuliziaji wa dawa za kuua mazalia ya mbu kwenye mabwawa ya maji na maeneo yenye mazalia ya mbu. Zoezi la kuua mazalia ya mbu lilifanywa na timu ya maafisa afya wa jiji la Dodoma.
Afisa Afya wa Jiji la Dodoma Abdalah Mahia alisema, kazi ya uangamizaji wa mazalia ya mbu katika mabwawa, mashimo ya maji taka na maeneo yote ambayo mbu wanaweza wakataga mayai. Alisema dawa hizo hazina kemikali hivyo basi, hazina madhara kwa binadamu. Akasisitiza wananchi kuchukua dawa hizo na kwenda kuzitumia kwenye mazingira ya majumbani kwao ili kutokomeza mbu. Lengo kuu ikiwa ni kujikinga na magonjwa ya malaria, dengue na mbu wanaosababisha mabusha na matende.
Tuko katika mkakati wa kutokomeza magonjwa hayo na wananchi wanatakiwa kuchukua dawa hizo kwa ajili ya kwenda kutumia majumbani kwao.
Afisa Afya wa Jiji pia alitahadharisha wananchi kuwa Dodoma kwa sasa kuna tatizo la ugonjwa wa sumukuvu, ambao husababishwa na vyakula vya nafaka kuweka ukungu (fangasi).
Utaratibu uliowekwa na Jiji ni watu wote kukagawiwa dawa na kuua mazalia ya mbu kupitia kwa mabalozi wao.
Mapema akiongea na wananchi wa Kata ya Miyuji, Afisa Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu Dickson Kimaro aliwashukuru wananchi wa Miyuji kwa kujitokeza kwa wingi kufanya usafi. Katika zoezi hilo kazi kubwa ilifanyika kusafisha mazingira ya eneo la Makaburi ya Wahanga. Eneo hilo lilisafishwa kwa kuondolea takataka na vichanga vilivyokuwa vinazunguka mazingira hayo na hata kuwa sehemu ya maficho ya vibaka.
Kimaro aliwakumbusha wananchi kuwa usafi ni kila jumamosi na usafi unatakiwa kufanyika mita tano kuzunguka maeneo ya makazi na sehemu za biashara. Lengo ikiwa ni kuweka jiji letu safi na kujiepusha na magonjwa mbali mbali yakiwemo yale ya milipuko.
Wananchi wa Kata ya Miyuji wakishiriki usafi wa kila Jumamosi, hapa wakifanya usafi kwenye Makaburi ya Wahanga
Umati mkubwa wa wananchi wa Kata ya Miyuji walioitikia mwito wa kufanya usafi siku ya jumamosi wakiwa na vifaa mbalimbali vya kufanyia usafi.
Zoezi la kufanya usafi likiendelea kwenye Makaburi ya Wahanga Miyuji.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.