• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Jiji la Dodoma laibuka tena kinara wa Mapato

Imewekwa tarehe: January 19th, 2019

Halmashauri 33  kati ya Halmashauri 185 zimeweza kukusanya Mapato ya Ndani kwa kiwango cha asilimia 50 na zaidi ya makisio ya mwaka wa fedha 2018/19 huku  Halmashauri 21 zikiwa zimefanya vibaya kwa kukusanya chini ya asilimi 20 ya makisio yake kwa mwaka.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemeni Jafo alipokuwa  akitoa taarifa ya Mapato ya Ndani ya Halmashauri kwa robo ya pili ya mwaka.

Alisema katika Halmashauri 33 zilizokusanya asilimia 50 na zaidi zimo Halmashauri za  Majiji tatu zikiongozwa na Jiji la Dodoma, Manispaa ni mbili zikiongozwa na Manispaa ya Iringa, Halmashauri za Miji nane zikizongozwa na Mji wa Geita na Halmashauri za Wilaya ni ishirini zikiongozwa na Halmashauri ya Wilaya ya Geita.

“Uchambuzi unaonyesha kuwa katika Majiji 6, Jiji la Dodoma linaongoza kwa kukusanya asilimia 59 ya makisio na Jiji la Tanga limekuwa la mwisho kwa kukusanya asilimia 33 ya makisio” alisema.

Aidha, Manispaa ya Iringa imeongoza katika kundi la Manispaa kwa kukusanya asilimia 64 ya makisio ambapo Manispaa ya Lindi imekuwa ya mwisho katika kundi hili kwa kukusanya asilimia 20 ya makisio.

Jafo aliongeza kuwa kwa upande wa Halmashauri za Miji, Halmashauri ya Mji wa Geita imeongoza kwa kukusanya asilimia 84 ya makisio na Halmashauri ya Mji wa Nanyamba imekuwa ya mwisho katika kundi hili kwa kukusanya asilimia 9 tu ya makisio,

Alisema Katika kundi la Halmashauri za Wilaya, Halmashauri ya Wilaya ya Geita imeongoza kwa kukusanya asilimia 78 ya makisio ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu imekuwa ya mwisho kwa kukusanya asilimia 6 tu ya makisio.

Kwa kuzingatia wingi wa makusanyo ya mapato ya  Halmashauri Jafo alibainisha Halmashauri iliyoongoza ni Jiji la Dodoma ambalo limekusanya Shilingi Bilioni 40.12 na Halmashauri iliyokusanya kiasi kidogo cha fedha ni Halmashauri ya Wilaya ya Momba ambayo imekusanya shilingi milioni 105.04.

Waziri Jafo pia alibainisha Mkoa ambao Halmashauri zake zimekusanya mapato kwa kuzingatia wingi wa mapato kuwa ni Mkoa wa Dar es salaam ambao kwa jumla Halmashauri zake zimekusanya shilingi bilioni 77.4 na Mkoa wa Mwisho ni Katavi ambao Halmashauri zake zimekusanya shilingi bilioni 2.4 tu.

Alisema katika Mkoa uliokusanya vizuri kwa kuzingatia asilimia ya makusanyo ni Mkoa wa Geita, Halmashauri zake zimekusanya asilimia  56.4 ya makisio ya mwaka ukifuatiwa kwa karibu na Mkoa wa Dodoma uliokusanya asilimia 55.9 ya makisio yake na Mkoa wa mwisho kwa kigezo hicho ni Mkoa wa Mtwara ambao umekusanya asilimia 15 ya makisio yake ya mwaka.

Wakati huo huo Waziri Jafo amewataka wakurugenzi wote ambao Halmashauri zao hazikufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato kwa kukusanya chini ya asilimia kumi ya makisio yake kwa kipindi cha nusu mwaka kujieleza na kujitathimini na kuhakikisha wanaongeza bidii katika suala la ukusanyaji wa mapato.

“Halmashauri 9 kati ya 10 zilizofanya vibaya katika mwaka wa fedha uliopita zimefanikiwa kufanya vizuri katika kipindi cha nusu mwaka wa fedha 2018/19 kwa kukusanya zaidi ya asilimia 20 ya makisio yake” alisema .

Waziri Jafo pia aliwaagiza Wakurugenzi wote kuhakikisha takwimu zote za mapato katika mfumo wa LGRCIS zinafanyiwa usuluhisho na kutumwa katika mfumo wa IFMIS (Epicor) kwani taarifa zote za mapato na matumizi ya fedha zinatakiwa kutolewa kupitia mfumo huo.

Ulinganifu huu wa taarifa za mapato umelenga kuonesha jinsi kazi za ukusanyaji wa Mapato ya Ndani katika Mamlaka za Serikali za Mitaa inavyoendelea kusimamiwa vyema na takwimu hizi zinazotolewa ni kwa mujibu wa taarifa zilizofanyiwa usuluhisho na kutumwa katika mfumo wa IFMIS (Epicor).

Katika mwaka wa fedha 2018/19 Halmashaurti zilipangiwa kukusanya shilingi bilioni 735.6 kutoka kwenye vyanzo vyake vya ndani na hadi kufikia Disemba 31, 2018 Halmashauri zimekusanya shilingi bilioni 300 sawa na asilimia 41 ya makisio.

Kwa kipindi cha kwa mwaka wa fedha 2017/18 Halmashauri zilipanga kukusanya shilingi bilioni 687.3 na hadi kufikia Disemba, 2017 Halmashauri hizo zilikuwa zimekusanya sh bilioni 281.3 sawa na asilimia 41 ya makisio.

Takwimu hizi zinabainisha kuwa kuna ongezeko la Shilingi bilioni 18.7 kwa mwaka wa fedha 2018/19 ikilinganishwa na makusanyo kwa kipindi kama hiki kwa mwaka wa fedha 2017/18.


Chanzo: Tovuti ya OR-TAMISEMI (www.tamisemi.go.tz)

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.