• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Jiji la Dodoma lajivunia kupata hati safi kwa miaka mitatu mfululizo

Imewekwa tarehe: March 28th, 2024

Na. Dennis Gondwe, DODOMA

HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma inajivunia kupata hati safi kwa miaka mitatu mfululizo kutokana na ushirikiano uliopo baina ya wataalam na Baraza la Madiwani katika kusimamia na kudhibiti matumizi sahihi ya fedha.

Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Kitengo cha Uhasibu na Fedha Halmashauri ya Jiji la Dodoma, CPA. David Rubibira alipokuwa akiongelea mafanikio ya serikali ya awamu ya sita kwa miaka mitatu ofisini kwake.

CPA. Rubibira alisema “kwa bahati nzuri kwa kipindi cha uongozi wa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Halmashauri ya Jiji la Dodoma imekuwa ikipata hati safi kwa miaka mitatu mfululizo. Hati inaangalia maeneo yafuatayo. Ukaguzi wa hesabu zilizowasilishwa na ukaguzi wa vitabu vilivyofanya malipo, nyaraka, viambata vyote na mchakato wa ukusanyaji mapato kama ulizingatia sheria, kanuni na taratibu. Hivyo, hati safi inatokana na muunganyiko wa hesabu kwamba umefuata viwango vya kimataifa na kuonesha ukweli” alisema CPA. Rubibira.

Alisema kuwa mafanikio hayo yanatokana na ushirikiano baina ya wataalam na Baraza la Madiwani. “Wataalam wanawajibu wa kufuata sheria, kakuni na taratibu za fedha wanapotekeleza majukumu yao na waheshimiwa madiwani wanawajibu wa kuisimamia halmashauri ili iweze kutekeleza majukumu yake. Hivyo, ushirikiano huu ndio unapelekea halmashauri kupata hati safi” alisema CPA. Rubibira.

Mafanikio mengine alitayaja kuwa ni katika eneo la ukusanyaji mapato ya ndani. “Mwaka wa fedha 2021/2022 halmashauri ilikisia kukusanya jumla ya shilingi 43,616,465,99, lakini iliweza kukusanya makusanyo halisi shilingi 44,279,552,980 sawa na asilimai 102. Mwaka wa fedha 2022/2023 halmashauri ilikamisia kukusanya shilingi 55,127,359,997 lakini iliweza kukusanya makusanyo halisi shilingi 44,639,819,472.12 sawa na asilimia 81. Mwaka 2023/2024 halmashauri ilikamsimia kukusanya shilingi 58,640,360,000 mpaka kufikia mwezi Machi, tumeshakusanya shilingi 32,760,459,121 sawa na asilimia 54.7. Kwa mikakati ambayo halmashauri imejiwekea kufikia tarehe 30 Juni, tunatarajia kuwa tumefikisha asilimia 100 ya makusanyo halisi” alisema CPA. Rubibira kwa uhakika.

Akiongelea mapokezi ya fedha za miradi ya maendeleo, alisema kuwa shilingi 29,654,533,199 zilipokelewa kutoka serikali kuu na wadau wa maendeleo. “Fedha hizo zilitekeleza miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa hospitali ya wilaya, vyumba vya madarasa, ujenzi wa shule, vituo vya afya, zahanati, nyumba za watumishi na matundu ya vyoo. Fedha hizo zilisaidia sana katika kuchochea maendeleo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

Akiongelea ukusanyaji wa mapato ya ndani alisema kuwa yanakusanywa vizuri. “Ndugu waandishi wa habari, ukusanyaji wa mapato ya ndani unakwenda vizuri. Asilimia 40 inatumika kuendesha halmashauri na asilimia 60 inatumika kutekeleza miradi ya maendeleo. Kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo tumeweza kutenga jumla ya asilimia 60 ya mapato ya ndani tuliyokusanya kwenda kwenye miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na asilimia 10 kwenye mfuko wa maendeleo ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu. Fedha za miradi ya maendeleo zimepekwa kwenye uchangiaji wa ujenzi wa barabara, kujenga vituo vya afya, madarasa na zahanati, ofisi za kata na mitaa. Hivyo, unaweza kuona kwa kiasi gani mapato ya ndani yamechangia kuleta maendeleo katika kipindi cha miaka mitatu” alisisitiza CPA. Rubibira.

Mkuu huyo wa Kitengo cha Fedha na Uhasibu aliwashukuru wananchi kwa kulipa kodi na tozo za halmashauri kwa hiari na kwa wakati. Aliahidi kuwa halmashauri itaendelea kutoa elimu kupitia vyombo vya Habari, matangazo na mikutano mbalimbali ili wananchi wapate elimu ya aina ya kodi na tozo za halmashauri wanazotakiwa kulipa ili waweze kulipa kwa hiari. “Hivyo, niwasihi wananchi kuendelea kulipa kodi kwa hiari, shughuli zote za maendeleo mnazoziona katika jamii ni matokeo ya kodi zenu. Wananchi mkiona wanafunzi wanaenda kwenye shule nzuri, madarasa mazuri, wanakalia madawati, wakienda hospitali huduma nzuri, dawa zipo mashine za vipimo zipo, ndiyo matunda ya ulipaji kodi” alisema CPA. Rubibira kwa tabasamu.

Aidha, aliwataka kudai risiti ya mashine ya kielekroniki (EFD) wanaponunua bidhaa. “Ndugu waandishi wa habari, nisisitize kwa wananchi wanaponunua bidhaa kuhakikisha wanapewa risiti za kielektroniki (EFD) na kama wanalipa tozo za halmashauri wahakikishe wanapata risiti ya POS” alisisitiza CPA. Rubibira.

Kitengo cha Uhasibu na Fedha kina jukumu la kukusanya maduhuli ya serikali na kusimamia matumizi kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.