• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Jiji la Dodoma laongoza tena Halmashauri zote kukusanya mapato

Imewekwa tarehe: October 22nd, 2019

Halmashauri ya Jiji la Dodoma imeendelea kuwa kinara wa ukusanyaji mapato na kuongoza Halmashauri zote nchini kwa kukusanya zaidi pato ghafi kiasi cha Sh Bilioni 13.1 kutoka katika vyanzo vya makusanyo yake ya ndani, licha ya kuwa kiasilimia wamekusanya asilimia 18 nyuma ya Jiji la Dar es Salaam ambao kufikia tarehe 30 Septemba, 2019 walikuwa wamefikia asilimia 38..

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jafo alipokuwa akitoa tathmini ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri zote nchini kwa kipindi cha Julai – Septemba, 2019 (Robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2019/2020).

Akifafanua zaidi, Mhe. Jafo alisema kuwa katika kuzipima Halmashauri zote kwa pamoja Halmashauri ya Jiji la Dodoma imekusanya mapato mengi zaidi kuliko Halmashauri zote kwa kukusanya shilingi Bilioni 13.10 na Halmashauri ya Buhigwe imekuwa ya mwisho kwa kukusanya shilingi Milioni 35.15.

Aidha, Halmashauri ya Wilaya ya Msalala imekuwa ya kwanza Kitaifa katika ukusanyaji wa mapato kiasilimia, kwa kukusanya asilimia hamsini na mbili (52%)  ya makisio ya mapato ya ndani kwa kipindi cha robo ya kwanza ya  mwaka wa fedha 2019/20 huku Halmashauri ya Kyerwa ikiwa ya mwisho kwa kukusanya asilimi tatu tu ya makisio yake.

Alisema Halmashauri ya Wilaya ya Msalala imefanikiwa kukusanya mara mbili ya malengo  ya robo ya kwanza ambapo kila Halmashauri ilitakiwa kukusanya si chini ya asilimia 25 ya makisio ili kukamilisha asilimia 100 kwa robo nne za mwaka wa fedha.

Waziri Jafo alieleza kuwa Bajeti iliyoidhinishwa ya mapato ya ndani ya Halmashauri zote nchini kwa mwaka wa fedha 2019/20 ni shilingi Bilioni 765.48; Katika kipindi cha robo ya kwanza (Julai hadi Septemba, 2019) Halmashauri zimekusanya jumla ya shilingi bilioni 166.24 sawa na asilimia 22 ya makisio ya mwaka.

Alieleza kuwa, “Katika kipindi hiki Halmashauri zilipaswa kukusanya asilimia 25 ya makisio yake ya mwaka lakini Halmashauri hamsini na nne tu (54) ndio zilizofanya vizuri kwa kukusanya zaidi ya asilimia 25 ya bajeti zao na Halmashauri 121 hazikuweza kufikisha asilimia 25 ya mapato yake”.

Pia Mhe Jafo aliongeza kuwa katika ngazi ya Mikoa, Mkoa wa Rukwa umeongoza kwa kukusanya wastani wa asilimia thethini na moja (31) ya makisio ya Halmashauri za Mkoa huo, huku Mkoa wa Mwisho ukiwa ni Mtwara ambao Halmashauri zake zimekusanya wastani wa asilimi kumi na tatu (13) ya makisio yake.

Aliongeza kuwa katika kipengele hicho cha Mikoa, kwa kuzingatia wingi wa mapato Mkoa ambao unaongoza kwa kukusanya mapato ya ndani kwa wingi ni Mkoa wa Dar es salaam ambao umekusanya shilingi Bilioni 39.53 na Mkoa wa Mwisho katika wingi wa ukusanyaji wa mapato ni Mkoa wa Kigoma ambao umekusanya shilingi bilioni 2.12.

Akisoma mchanganuo wa ukusanyaji wa mapato kwa kuzingatia aina ya Halmashauri na vigezo mbalimbali Mhe. Jafo amesema kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam imeongoza kundi la Halmashauri za Majiji kwa kukusanya mapato kwa asilimia 38 ya makisio yake ya mwaka huku Halmashauri ya Jiji la Dodoma ikiwa ya mwisho katika kundi hili kwa kukusanya kwa asilimia kumi na nane (18%) ya makisio yake ya mwaka.
Mhe. Jafo alitaja Halmashauri za Majiji zilizokusanya mapato ya ndani kwa kigezo cha wingi (Ghafi) kuwa Jiji la Dodoma limeongoza kwa kukusanya shilingi bilioni 13.098 na Halmashauri ya Jiji la Mbeya imekuwa ya mwisho katika kundi hili kwa kukusanya shilingi bilioni 2.74 tu.

Hali kadhalika Jafo alitaja Manispaa iliyoongoza kundi la Halmashauri za Manispaa kwa kigezo cha asilimia kuwa ni Manispaa ya Sumbawanga ambayo imekusanya kwa asilimia arobaini na mbili (42) na Manispaa ya mwisho katika kigezo hiki ni Manispaa ya Kigoma ambayo imekusanya kwa asilimia tisa tu ya makisio yake kwa mwaka.

“Katika kigezo cha wingi wa mapato kundi hili linaongozwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ambayo imekusanya shilingi bilioni 13.05 huku Manispaa ya Kigoma ikiwa ya mwisho tena kwa kukusanya kiasi kidogo cha fedha cha shilingi milioni 235.11" alisema Jafo.

Akielezea kipengele cha Halmashauri za Miji Jafo alisema kuwa Mji wa Tunduma umeongoza kwa kukusanya kwa asilimia thelathini na tisa (39%) na Halmashauri ya Mji wa Nanyamba imekua ya mwisho kwa kukusanya asilimia nne (4%) ya makisio ya mapato yake ya ndani kwa mwaka.

Mhe. Jafo alisema kuwa Halmashauri ya Mji wa Geita imeendelea kuongoza kwa wingi wa mapato katika Halmashauri za Miji kwa kukusanya shilingi bilioni 2.34 na Halmashauri ya mwisho ni Mji wa Nanyamba ambayo imeksuanya shilingi milioni 74.72.

Wakati huo huo Jafo amezitaja Halmashauri za Wilaya zilizofanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato kiasilimia kuwa ni Halmashauri ya Msalala ambayo imekusanya kwa asilimia hamsini na mbili (52%) na Halmashauri ya Kyerwa imekuwa ya mwisho kwa kukusanya asilimia tatu (3%) ya makisio ya mapato ya ndani kwa mwaka.

Upande wa wingi wa mapato Mhe. Jafo alitaja Halmashauri ya Wilaya iliyoongoza katika kundi hili kuwa ni Halmashauri ya Chalinze ambayo imekusanya shilingi bilioni 2.05 na ya mwisho ni Halmashauri ya Buhigwe iliyokusanya shilingi milioni thelathini na tano (35) tu.

Jafo alisema kuwa katika matumizi ya mapato ya vyanzo vya ndani katika taarifa hii ya robo ya kwanza haionyeshi picha halisi ya uchangiaji wa mapato hayo katika shughuli za maendeleo kwenye sekta ya Elimu, Afya na Maji.

“Uchambuzi kamili wa uchangiaji wa kila halmashauri katika miradi ya maendeleo utafanyika katika robo ya pili na mwisho wa mwaka wa fedha 2019/20 lakini kila Halmashauri ifanye jitihada kuhakikisha inachangia mapato ya ndani kulingana na asilimia inayopaswa kuchangiwa kwa mujibu wa bajeti zake” Alifafanua Jafo.

Vilevile, Mhe. Jafo alieleza kuwa katika kipindi cha Julai - Septemba,2019 Halmashauri zilitumia shilingi Bilioni 40.88 kati ya shilingi bilioni 340.68 zilizokasimiwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo sawa na asilimia 12.

Mhe. Jafo alikumbushia matumizi sahihi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) hususani mifumo ya kielektroniki ya ukusanyaji wa mapato, mashine za kukusanyia mapato (PoS) na mifumo ya Kielektroniki ya kutolea taarifa.

Alimalizia  kuwataka viongozi kuweka mikakati madhubuti ya kukusanya mapato kutoka kwenye vyanzo vipya vinavyobuniwa na Halmashauri zao.


Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.