OFISI ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma imepokea ugeni kutoka nchini Italia ambao ni asasi ya kiraia inayojulikana kama CMSR chini ya Mkurugenzi Mtendaji ndugu Alberto Benvenun inayojihusisha na masuala ya kijamii katika sekta mbalimbali kama vile afya, elimu, kilimo na maji ambapo kimsingi sekta hizo zimekkuwa na changamoto kubwa katika utoaji wa huduma zake katika jamii.
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma ndugu Joseph Mafuru pamoja na Mstahiki Meya wa Jiji hilo Profesa Davis Mwamfupe walikutana na ujumbe wa asasi hiyo ya kiraia kwa lengo la kutambua shughuli wanazozifanya katika kusaidia jamii kwenye sekta mbalimbali ambapo jiji la Dodoma limekuwa ni moja ya maeneo yanayonufaika na asasi hii ya kiraia kutoka nchini Italia.
CMSR ni taasisi binafsi yenye makao makuu yake katika mji wa Livomo nchini Italia ambapo kwa muda mrefu imejikita katika kusaidia wananchi wanoishi katika mazingira magumu kwa kutoa huduma za maji, afya na elimu ambapo katika maeneo mengi imekuwa ngumu wananchi kupata huduma hizi kwa uhakika.
Mkurugenzi Mtendaji wa asisi hii ya kiraia ya CMSR ndugu Alberto Benvenun ameeleza maeneo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma yaliyonufaika katika miradi yao kuwa ni Kata ya Zuzu ambapo waliweza kufunga mabomba ya maji, wamefunga mitambo ya umeme wa jua katika vituo vya afya katika maeneo ya Chamwino na kuwa wana utaratibu wa kuwalipia ada za shule kwa wanafnuzi wenye uhitaji. Mpaka sasa zaidi ya wanafazui 43 wamewalipia ada na zaidi ya wanafunzi 10 wamefikia hatua ya elimu ya Chuo Kikuu.
Mstahiki Meya Profesa Davis Mwamfupe ameahidi kuandaa utaratibu mzuri katika kikao cha Baraza la Madiwani kwa kuzitambua taasisi binafsi ambazo zinajishughulisha na masuala ya kijamii kaitka Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma Profesa Davis Mwamfupe akiongea wakati ugeni kutoka Italia ulipotembelea ofisi za Jiji la Dodoma kwa ajili ya ushirikiano hasa kwenye utoaji wa huduma za jamii.
Mazungumzo kati ya uongozi wa Jiji la Dodoma na CMSR yaliyofanyika ofisini kwa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.