Na. Fransisca Mselemu, DODOMA
HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imetoa mafunzo ya matumizi ya mfumo wa manunuzi wa kieletroniki (NeST) kwa lengo la kukuza uelewa kwa watumishi wa kada mbalimbali ikiwa ni utekelezaji wa sheria mpya ya manunuzi ya umma ya mwaka 2023.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Shule ya Sekondari Dodoma, Afisa Manunuzi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Josephat Ngumayo alisema kuwa mafunzo hayo ni muhimu sana kwasababu yatawasaidia watumishi katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi ambapo kwa sasa masuala yote ya manunuzi ni lazima yapitie kwenye mfumo wa NeST. “Mafunzo haya tunayatoa ikiwa ni utekelezaji wa sheria mpya ya manunuzi ya umma yam waka 2023 inayoelekeza manunuzi ya umma kufanyika kupitia mfumo wa kielektroniki wa NeST” alisema Ngumayo.
Nae mwezeshaji wa mafunzo hayo ambae pia ni Afisa Ugavi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba, Nasibu Lukas alisema "mfumo wa NeST umekuja kutatua changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikilalamikiwa hasa na wazabuni ambao wamekuwa wakidai kuwa kuna upendeleo katika utoaji wa zabuni. Hivyo, walimu msiogope kuutumia kupitia mafunzo haya mtauelewa vema".
Kwa upande wake Mwl. Stanley Mvuyekule kutoka Shule ya Sekondari Miyuji alisema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia kwenye kufanya manunuzi haraka. ''Kwa kweli mafunzo haya ya mfumo wa manunuzi wa kielekroniki yaani NeST yatasaidia sana kuondoa changamoto zilizokuwa zikitukabili katika utaratibu mzima wa manunuzi kwasababu kulikuwa na usumbufu hasa katika 'quotations', lakini mfumo huu umerahisisha sana kazi. Kazi zitafanyika kwa ufanisi na kwa taratibu zinazotakiwa'' alisema Mwl. Mvuyekule.
Nae Mwl. Rosemary Mark kutoka Shule ya Sekondari Mlimwa alisema mfumo utaweka uwazi na uwajibikaji. "Mfumo huu wa NeST utawasaidia walimu, wahasibu na walimu wote kwa ujumla hasa katika mchakato wa kupata mafundi, wazabuni mbalimbali tofauti na siku za nyuma ambapo mfumo haukuwepo. Awali tulilazimika kuwafuata maofisini kwao au kuwapigia simu, lakini kupitia mfumo huu wanaomba wenyewe. Pia mfumo unakwenda kutatua changamoto ya ushindani wa bei. Vilevile, kutakuwa na uwazi katika kuwachagua
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.