AFISA Elimu Awali na Msingi Jiji la Dodoma, Prisca Myalla amesema Jiji la Dodoma mpaka kufikia tarehe 8 Januari,2024 limefanikiwa kusajili wanafunzi zaidi ya elfu kumi wa darasa la Awali na Msingi.
Hayo aliyasema alipotembelea shule ya msingi Nzughuni B na Chikole zilizopo jijini hapo kuangalia uzunduzi wa madarasa mapya na hali ya uandikishaji wa wanafunzi wa elimu ya awali na darasa la kwanza.
“Ni jambo la kumshukuru Mungu mpaka sasa halmashauri imefanikiwa kusajili wanafunzi zaidi ya elfu kumi wa darasa la awali na msingi. Nawapongeza sana viongozi wa kata na mtaa kwa uhamasishaji pia nawapongeza wazazi kwa kutii wito na kuwapeleka watoto waliofikisha umri wa kwenda shule kujiandikisha shuleni, kila mtoto anahaki yakupata elimu na kwakulitambua hilo Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan amehakikisha anatoa elimu bure kwa watoto wetu ili kila mmoja apate fursa ya elimu niwaombe wazazi tuhakikishe tunaunga jitihada hizi za Rais wetu kwa kuhakikisha watoto wetu kweli wanaenda shule kusoma na sio kuishia mitaani” alisema Myalla.
Sambamba na hilo Myalla aliongezea kuwa kutakua na mafunzo ya mtaala mpya wa masomo kwa walimu wa shule ya awali na msingi.”Tunatarajia kuanza mafunzo ya walimu ndani ya wiki hii ili walimu wetu waendane na kasi za mtaala mpya
Kwa upande wake Rose Malembeka, Mwanafunzi kutoka shule ya Nzughuni B alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapa elimu bure na kuwajengea madarasa huku akiahidi hawatomuangusha watasoma Kwa bidii”Kwa niaba ya wanafunzii wenzangu namshukuru sana mama Samia kwa kutujengea madarasa hatuna cha kumlipa zaidi tunaahidi tutasoma kwa bidii kuhakikisha tunayafika malengo yetu”.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.