HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imeahidi kuwashonea sare wanafunzi wote wenye mahitaji maalum katika shule ya msingi Mpunguzi ili wasitofautiane na wanafunzi wengine na kuchochea maendeleo ya kitaaluma kwa watoto hao.
Ahadi hiyo ilitolewa na Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Mhe Prof. Davis Mwamfupe alipoongoza timu ya wageni kutoka Jiji la Linz la nchini Austria walipotembelea shule ya Msingi Mpunguzi jana.
Meya Prof. Mwamfupe alisema kuwa wanafunzi wenye mahitaji maalum wana haki ya kupata elimu kama wanafunzi wengine.
Wanafunzi wenye mahitaji maalum wana changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na changamoto ya sare.
“Nitawashonea sare wanafunzi wote 28 wenye mahitaji maalum katika shule hii” alisema Prof. Mwamfupe.
Alisema sare hizo zitakuwa kama motisha na zitasaidia kuchochea maendeleo ya taaluma kwa wanafunzi hao shuleni hapo.
Akiongelea ujenzi wa darasa la wanafunzi wenye mahitaji maalum katika shule hiyo, Prof. Mwamfupe aliwataka wananchi kuanza ujenzi huo ili kuwapa haki wanafunzi hao ya kusoma katika mazingira rafiki.
“Wito wangu kwenu ndugu zangu, Mhe. Diwani, anzeni ujenzi wa darasa hilo na halmashauri ya Jiji itaunga mkono juhudi zenu” alisema Prof. Mwamfupe.
Awali, Mstahiki Meya wa Jiji la Linz kutoka nchini Austria, Klaus Luger alielezea kufurahishwa kwake na mapokezi waliyopata katika shule hiyo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.