HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imeanza kutoa elimu na mafunzo kwamakundi ya wadau kuhusiana na zoezi la kitaifa la uwekaji wa Anwani za Makazina Postikodi katika nyumba na mitaa yote 222 ya Jiji hilo ambapo kundi lakwanza limejumuisha Madiwani wa Kata zote 41 za Halmashauri hiyo.
Semina hiyo imetolewa Machi 11,2022 katika ukumbi Mkuu wa Mikutano wa Jiji hilo ambapo iliendeshwa na wajumbewa Kamati inayosimamia zoezi ikiongozwa na mratibu wa Joseph Nkuba.
Akitoa muhtasari wa maendeleo yakazi hiyo kwa madiwani hao, Nkuba alisema tayari uzinduzi rasmi ulishafanywa naMkuu wa Wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri na kwamba wameshaajiriwa vijana 300watakaofanya kazi ya kukusanya taarifa za kila nyumba na kuzisajili katikamfumo wa anwani pamoja na kusajili barabara na mitaa yote.
“Sasa zoezi linalofuatia nikutambua namba za nyumba kwa mitaa yote na kuchukua taarifa za wakazi nakuzisajili katika mfumo ambalo litaanza Machi 14, 2022 na kukamilika April 172022” alisema.
Wakizungumza kwenye semina hiyomadiwani wa jiji la Dodoma walisema kuwa mradi wa uwekaji anwani za makazilitawawezesha wananchi wao kujiinua kiuchumi kwa kuwa utaleta maendeleo.
Meya wa Jiji la Dodoma MstahikiProf. Davis Mwamfupe aliwataka madiwani, watendaji, na wenyeviti wa mitaa ndaniya jiji hilo kuwa mabalozi wa kuwaelimisha wananchi ili zoezi hilo likamilikekwa wakati.
Aidha, amewataka wataalam kwaupande wao kuifanya kazi hiyo kwa uzalendo na wananchi kutoa taarifa sahihi kwaajili ya kuziweka kwenye mfumo na kuwezesha kutambulika kwa mitaa.
Kwa upande wake Israel Mwansasuambaye ni diwani wa kata ya Kikuyu Kaskazin alisema kuwa, mradi huo kwa kuwaunawagusa watanzania wote unatakiwa kila mmoja kuhakikisha anakuwa mlinzi wakulinda miundombinu yake.
Semina hiyo itafanywa kwa sikumbili ambapo kundi linalofuata ni watendaji wa kata na mitaa pamoja vijana 300waliopatiwa ajira ya muda ya kufanya kazi hiyo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.